Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mbeya, Godphrey
Zambi ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Mbozi Mashariki alisema sherehe hizo
zinatarajiwa kufanyika Februari 2, Mwaka huu.
Baadhi ya
waandishi wa habari wakimsikiliza
Mwenyekiti wa CCMmkoa wa Mbeya
Charles
Mwakipesile Mjumbe wa NEC
Mwenyekiti
wa CCM Mkoa wa Mbeya, Godphrey Zambi ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Mbozi
Mashariki akiwa na katibu wa ccm mkoa wa Mbeya Maganga Sengerema
RAISI wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dk. Jakaya Mrisho Kikwete ambaye pia ni
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Taifa anatarajiwa kuwa Mgeni rasmi katika
sherehe za maadhimisho ya Miaka 37 ya kuzaliwa kwa chama hicho zitakazofanyika
kitaifa Mkoani Mbeya.
Akitoa
taarifa kwa waandishi wa Habari katika
Mkutano uliofanyika katika Ofisi za Chama hicho Mkoa zilizopo Sokomatola Jijini
Mbeya, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mbeya, Godphrey Zambi ambaye pia ni Mbunge wa
Jimbo la Mbozi Mashariki alisema sherehe hizo zinatarajiwa kufanyika Februari
2, Mwaka huu.
Zambi
alisema maadhimisho ya miaka 37 ya kuzaliwa kwa Chama cha mapinduzi ambayo
yatafanyika kitaifa Mkoani Mbeya na Raisi Kikwete kuwa Mgeni rasmi yataanza
majira ya saa 12 alfajiri kwa kufanya
matembezi ya Mshikamano.
Alisema
matembezi hayo yataanzia katika viwanja vya John Mwakangale (nanenane) na
kuishia katika Ofisi za Chama Mkoa eneo la Sokomatola yakihusisha Viongozi wa
Chama na Wananchi mbali mbali wa Mkoa wa Mbeya na mikoa jirani.
Aliongeza
kuwa baada ya matembezi hayo Wananchi na viongozi watapata mapumziko kidogo na
kisha kuendelea na sherehe katika Viwanja vya Kumbu kumbu ya Sokoine
zitakazoanza majira ya Saa nane Mchana.
Aidha
mwenyekiti huyo alikipongeza Chama cha Mapinduzi Taifa kwa kuuteua Mkoa wa
Mbeya kuwa Mwenyeji wa Sherehe hizo ambazo hazijawahi kufanyika Mkoani Mbeya
tangu kuzaliwa kwa Chama hicho Mwaka 1977.
Alisema ni
fursa pekee ya wakazi wa Mkoa wa Mbeya ya kukutana na Raisi Kikwete ambaye
ataweza kuwaeleza wananchi mafanikio yaliopatikana Mkoani Mbeya tangu kuzaliwa
kwa Chama hicho hadi sasa.
Aliyataja
baadhi ya mafanikio kuwa ni pamoja na Ongezeko la Vyuo vikuu ambavyo awali
havikuwepo Mkoani Mbeya sambamba na kuimarishwa kwa miundombinu hususani ujenzi
wa barabara za Lami ambazo Mbunge wa Chadema Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi anadai
yeye ndiye amejenga.
Alisema
mafanikio mengine wanayopaswa kujivunia wakazi wa Mkoa wa Mbeya ni pamoja na
sekta ya Elimu, Afya, Maji na Umeme ambapo sehemu kubwa ya Mkoa wa Mbeya wenye
wakazi zaidi ya Milioni Mbili na Wanachama wa chama hicho zaidi ya Laki tatu
wakipata huduma bora za kijamii.
Zambi
aliongeza kuwa kutokana na kufanyika kwa sherehe za maadhimisho ya miaka 37 ya
kuzaliwa kwa CCM Mkoani Mbeya, Mkutano wa Halmashauri Kuu ya Chama hicho ambao
awali ulitarajiwa pia kufanyika Mkoani hapa umeahirishwa na kuhamishiwa mkoa
mwingine ambao haukutajwa.
Wakati huo
huo Mwenyekiti huyo alizungumzia mgogoro unaoendelea ndani ya Chama cha
Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA) kwamba CCM haihusika nao kama baadhi ya watu
wanavyodai.
Alisema
Chama cha Mapinduzi hakifurahii migogoro ya vyama vya upinzani kwa sababu
vilianzishwa kwa lengo la kuikumbusha Serikali iliyopo madarakani pindi
inapofanya vibaya au kujisahau katika kufanya shughuli za kuwaletea Maendeleo
Watanzania.
Alisema hata
ndani ya CCM matatizo kama hayo hutokea lakini humalizwa kupitia vikao halali
vya chama na kuendelea na shughuli zake kama kawaida na sio kukimbilia kwenye
vyombo vya habari kutangaziana mabaya.
No comments:
Post a Comment