EBENEZA MARCH 9 2014

EBENEZA MARCH 9 2014

Thursday, January 16, 2014

Athuman Chuji aitwa kucheza soka Nepal

 

Kiungo wa timu ya Yanga, Athuman Idd ‘Chuj 
0
Shar

KIUNGO mkabaji wa zamani wa Yanga ambaye sasa anacheza soka la kulipwa Nepal nchini India, Godfrey Bonny amemuita kiungo wa timu hiyo, Athuman Idd ‘Chuji’ nchini humo.
Kauli hiyo ameitoa baada ya kupata taarifa ya kusimamishwa kiungo huyo hivi karibuni kwa kile kinachodaiwa ni utovu wa nidhamu aliounyesha kwenye timu hiyo katika mechi ya Nani Mtani Jembe na kumalizika kwa Yanga kufungwa mabao 3-1 dhidi ya Simba.

Akizungumza na Mwanaspoti, Bonny alisema anaamini kiungo huyo ana uwezo mkubwa wa kucheza soka la kulipwa kama alivyokuwa yeye ndani ya uwanja.
Bonny alisema Chuji asikatishwe tamaa kwa hali hiyo iliyotokea na badala yake aendelee kufanya mazoezi kwa bidii ili kiwango chake kisishuke.
Aliongeza kuwa anashangazwa na aina ya soka la Tanzania ambalo wenyewe wanataka mchezaji kila wakati awe kwenye kiwango cha juu bila kufahamu mwili wa binadamu unachoka ukitumika sana kama iliyotokea kwa Chuji.
“Nimepata taarifa za Chuji kusimamishwa na Yanga, ninashangazwa na mfumo wa uendeshaji wa viongozi wa soka ambao timu ikifungwa tu, basi wanatafuta mchawi kwa kusimamisha wachezaji kwa madai ya kuchukua rushwa kitu ambacho siyo sahihi.
“Nimtoe hofu Chuji kwa kumwambia aendelee kufanya mazoezi kwa bidii ili kiwango chake kisishuke na kama akifukuzwa kabisa basi nitamuita huku Nepal kuja kucheza soka la kulipwa nafasi zimejaa tele.
“Ninaamini hataniangusha kutokana na na uwezo wake ndani ya uwanja anacheza soka la akili na nguvu nyingi ni kati ya wachezaji ninaowakubali nchini,” alisema Bonny anayecheza katika klabu ya Saraswot Youth Club.
SOURCE: MWANASPORT

No comments:

Post a Comment