EBENEZA MARCH 9 2014

EBENEZA MARCH 9 2014

Monday, January 27, 2014

CHADEMA YABAINIKA KUWA UWEZO WAKE NI MDOGO KUSHIKA DOLA YASEMEKANA UTAWALA WAKE NI WA KIDIKTETA



Chama cha mapinduzi ( CCM) manispaa ya Moshi mkoani Kilimanjaro kimeendelea kusisitiza kuwa chama cha demokrasia na maendeleo, CHADEMA hakitaweza kushika dola kutokana na mfumo wake wa utawala kuwa mbovu....
Kauli hiyo ilitolewa jana na mwenyekiti wa CCM manispaa ya Moshi, Elizabeth Minde wakati alipokuwa akimnada mgombea wa udiwani wa kata ya Kiboriloni kwa tiketi ya chama hicho, Willy Adriano...
Mwenyekiti huyo alisema migogoro inayoendelea ndani ya chama hicho ni ishara ya utawala mbovu unaotokana na udikteta, udini na ukabila, hivyo chama hicho kupewa dola ni kuhatarisha amani ya nchi hii ambayo imekuwa nembo ya taifa hili kimataifa...
Alisema CCM imejipanga vya kutosha kupata ushindi katika uchaguzi huo huku akiwatahadharisha wanaoibeza CCM kuwa tayari kuingia aibu ufikapo februari 9 maka huu...

"Ili mwananchi aweze kupata maendeleo tunahitaji kupata kiongozi makini ambaye ataweza kuwaletea wananchi maendeleo, hivyo nawaomba wananchi wa kata ya Kiboriloni wamchague Willy Adriano, CCM ushindi unakuja"..Alisema Minde
Kwa upande wake katibu mwenezi wa CCM mkoa, Michael Mwita, alisema kazi ya CCM ni kuisimamia serikali katika kutekeleza shughuli za kimaendeleo kutokana na ilani ya chama hicho.
"Asilimia 90 ya wakazi wa Kiboriloni wanakabiliwa na changamoto lukuki, huwezi kuwa na mbunge ambaye ana maslahi yakwake.Kuna wapanda mlima wamekuwa wakinyanyasika na malipo yao duni, lakini imekuwa ngumu kwa mbunge huyo kuwatetea vijana hao" Alisema Mwita
Aliongeza kuwa mbunge huyo tangu achaguliwe mwaka 2000 hakuna maendeleo yoyote aliyowaletea wananchi wa Moshi pamoja na kutoa ahadi lukuki ikiwemo ahadi ya kurudisha soko la Kiboriloni ambalo kwa sasa limehamishwa.
Alisema mbunge huyo hana nia ya dhati ya kuwakomboa wananchi wake tofauti na anavyodai katika majukwaa ya siasa na kuongeza kuwa mwaka 2010 aliwaahidi wamachinga kuwa endapo watamchagua na kumpa halmashauri atahakikisha machinga hawanyanyaswi huku akiahidi kuwajengea machinga complex, ahadi ambayo haijatekelezwa hadi sasa.




No comments:

Post a Comment