EBENEZA MARCH 9 2014

EBENEZA MARCH 9 2014

Sunday, November 10, 2013

WAJUMBE WA BARAZA LA USALAMA UN WALAANI SHAMBULIO LA MOGADISHU



Wajumbe wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, wamelaani vikali shambulio la bomu lililofanyika Ijumaa kwenye mji mkuu wa Somalia, Mogadishu. 


Tayari kundi la kigaidi la Al-Shabaab limedai kuhusika na hujuma hiyo iliyosababisha vifo vya watu zaidi ya watu 11 na wengine kadhaa kujeruhiwa.  Baraza la Usalama limesema linaunga mkono kwa dhati mchakato wa amani na maridhiano nchini Somalia.




Aidha baraza hilo limesema linaunga mkono jitihada za kimataifa za kuondoa tishio la kundi la kigaidi la Al Shabaab nchini Somalia na kwenye eneo lote. Wakati huo huo Ethiopia imesema itatuma wanajeshi wake nchini Somalia kujiunga na kikosi cha Umoja wa Afrika chenye askari elfu 18.
Hayo yamedokezwa na Waziri Mkuu wa Ethiopia Hailemariam Desalegn wakati alipokutana na Naibu Rais wa Kenya William Ruto mjini Addis Ababa jana Jumamosi.
Hivi karibuni makamanda wa kikosi hicho walisema hawana askari na vifaa vya kutosha kuangamiza kabisa waasi wa al Shabaab, ambao bado wanadhibiti baadhi ya maeneo ya kusini na kati mwa Somalia.

No comments:

Post a Comment