EBENEZA MARCH 9 2014

EBENEZA MARCH 9 2014

Sunday, November 10, 2013

IRANI YAFELI KUFIKIA MAKUBALIANO NA NCHI TAJIRI DUNIANI



Iran na mataifa yenye nguvu duniani, wameshindwa kufikia makubaliano hii leo Jumapili, kuhusu mpango wa Nyuklia wa Iran, licha ya mazungumzo ya muda mrefu mjini Geneva.
 
Rais wa Iran
Hali hiyo imeondoa matarajio ya makubaliano yaliyotarajiwa kwa muda mrefu katika msuguano huo wa muongo mmoja.
Hata hivyo wanadiplomasia wamesema maendeleo makubwa yamefikiwa katika siku tatu za majadiliano makali, na kwamba mazungumzo hayo yataanza tena mnamo Novemba 20.
Matumaini yaliongezeka baada ya wanadiplomasia wa juu duniani kuwasili mjini Geneva, kujiunga na mazungumzo hayo, lakini yalififia baada ya baada ya nyufa kuanza kuonekana miongoni mwa mataifa yenye nguvu baada ya Ufaransa kuonesha wasiwasi.
Makubaliano yanayotumainiwa yameonekana kama hatua ya mwanzo, kabla ya mazungumzo zaidi kuhusu makubaliano ya mwisho, na huenda yakaishuhudia Iran ikifungia juhudi zake za nyuklia kwa muda wa miezi sita, kama mbadala wa kuondokana na vikwazo ambavyo vimeharibu uchumi wake.

No comments:

Post a Comment