Wananchi wa Muaritania wanasubiri matokeo ya kura za kuwachagua wabunge
na viongozi wa serikali za mitaa, chama cha kiislamu ndicho kinachotazamiwa
kuongoza katika uchaguzi huo.
Takribani wananchi milioni 3.4 wamepiga kura jana jumamosi, jumla ya
wagombea 1500 kutoka vyama vya siasa 74 wamechuana kuwania viti 147 katika
bunge na viti 218 vya uwakilishi wa serikali za mitaa.
Licha ya wapinzani kupinga zoezi hizo,
limetamatika kwa amani bila kuripotiwa kwa ghasia zozote hadi hivi sasa.Rais wa nchi hiyo Mohamed Ould Abdel Aziz amesema uchaguzi huo ni ushindi katika kutafuta demokrasia ya kweli ndani ya Taifa hilo.
Rais Abdel Azizi aliingia madarakani baada ya mapinduzi ya mwaka 2008, na mwaka mmoja baadaye alishinda katika uchaguzi wa kidemokrasia, hata hivyo Taifa hilo limekuwa na hostoria ya utawala wa kijeshi toka kuanza kwa mfumo wa uchaguzi wa vyama vingi mwaka 1992.
No comments:
Post a Comment