EBENEZA MARCH 9 2014

EBENEZA MARCH 9 2014

Sunday, November 10, 2013

BUNGE LAUNDA KAMATI KUCHUNGUZA MGOGORO WA WAKULIMA NA WAFUGAJI NCHINI



Spika wa Bunge, Anne Makinda ameunda Kamati Teule ya Bunge, kuchunguza migogoro inayowahusisha wakulima, wafugaji na watumiaji wengine wa ardhi hapa nchini.
 
Spika wa bunge la Tanzania-Anne Makinda

Makinda ametangaza kamati hiyo ya wabunge watano hapo jana, muda mfupi kabla ya Bunge kuahirishwa, hatua ambayo ni utekelezaji wa uamuzi wa Bunge uliofanywa Novemba Mosi, mwaka huu.
Kamati hiyo teule itaongozwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji, Profesa Peter Msola na wajumbe Mwenyekiti wa Kamati ya Maendeleo ya Jamii, Jenista Mhagama na Magdalena Sakaya.




Wengine ni Mbunge wa Rombo, Joseph Selasini na Mbunge wa Simanjiro, Christopher Ole Sendeka. Makinda amesema uteuzi wake umezingatia uwakilishi wa vyama, uelewa wa tatizo na migogoro iliyopo nchini, uzoefu katika masuala ya kilimo na ufugaji na jinsia.
Amezitaja hadidu za rejea kuwa ni, kuchambua sera mbalimbali zinazohusiana na matumizi ya ardhi, ili kubainisha kasoro zilizopo na kuchunguza mikakati ya utekelezaji.
Nyingine ni kuchambua mikakati ya kulinda vyanzo vya maji, uharibifu wa mazingira, kutoa mapendekezo jinsi ya kuondoa migogoro na kudumisha uhusianao na utengamano kati ya wafugaji na wakulima.
Kuundwa kwa Kamati Teule ni utekelezaji wa Azimio la Bunge la Novemba 1, 2013, baada ya mjadala kuhusu mambo mawili, Operesheni Tokomeza Ujangili na Migogoro baina ya wakulima na wafugaji.


No comments:

Post a Comment