EBENEZA MARCH 9 2014

EBENEZA MARCH 9 2014

Saturday, November 16, 2013

BIN SLUM AMNG'ANG'ANIAKADO ASEMA BADO MCHEZAJI WA COASTAL


SHAABAN KADO

Mkurugenzi wa Ufundi wa Coastal Union, Nassor Bin Slum amesema kipa Shabani Kado anaendelea kubaki katika kikosi hicho.



Bin Slum alikuwa anazungumzia kuhusiana na Simba, jana kulizagaa taarifa kwamba kipa huyo yuko mbioni kujiunga na Simba.

Lakini Bin Slum alisisitiza kwamba kipa huyo ana mkataba na ataendelea kuichezwa Coastal

"Kado ana mkataba hapa, Simba hawawezi kuzungumza naye kabla ya kufika kwetu, hivyo Kado bado yuko Coastal," alisema Bin slum

Simba imekuwa ikihaha kusaka kipa ikiwa ni siku chache baada ya kumuacha kipa Juma Kaseja aliyekuwa nahodha wa timu hiyo kwa madai ya kuteremka kiwango.

No comments:

Post a Comment