VIGOGO wa soka nchini
Misri klabu ya Al Ahly wameshindwa kushawishi mamlaka ya kijeshi nchini
humo ili kuhamisha mchezo wao katika Uwanja wenye uwezo wa kuingiza watu
70,000 ambao sasa watalazimika kucheza mechi yao ya mkondo wa ili ya
fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Orando Pirates katika Uwanja
wa Arab Contractors.
Uwanja
huo wenye uwezo wa kubeba mashabiki 30,000 utapunguza madhara ya kuwa
na mashabiki wengi watukutu wa Al Ahly lakini Pirates sasa itabidi
wajipange vyema kutokana na nyasi za kuchezea kutokuwa vizuri.
Wiki
iliyopita Al Ahly walifanikiwa kuhamisha mechi hiyo jijini Cairo baada
ya mabingwa hao mara saba wa michuano hiyo kuwa wakicheza mechi zao
katika Uwanja wa El-Gouna uliopo nje ya mji wa Cairo kwa miezi kadhaa.
Mamlaka
ya kijeshi nchini Misri hawataki mechi yoyote kuchezwa katika mji mkuu
wan chi hiyo toka rais Mohamed Mursi alipoondolewa madarakani JUlai
mwaka huu kwa hofu ya kuogopa mkusanyiko mkubwa unaoweza kusababisha
machafuko.
No comments:
Post a Comment