Akizungumzia suala hilo,
Mwenyekiti wa Wazazi Mkoani Tanga Dkt
Edmund Mndolwa, alisema hayo katika ziara ya kuwashukuru kwa
kumchagua kwa kishindo katika nafasi hiyo ya kuwa
mwenyekiti wa Jumuiya hiyo na kutembelea wilaya zote 9 za
Mkoa wa Tanga.
Alisema imekuwa ni jambo
la kawaida kwa wenyeviti na Makatibu kufanya kazi kimazoea kwa kufanya kazi
zisizo eleweka kwa kigezo cha kuwa Chama Cha Mapinduzi tayari ni chama kikubwa
na kinapendwa na kuza hofu kwa mustakabali wa siasa za Tanzania.
Waziri Chizza aingilia kati mgogoro wa wakulima wa Chai wilayani Lushoto, mkoani Tanga
Na Ray Said, Bumbuli
WAZIRI
wa Chakula, Kilimo na Ushirika, Injinia Christopher
Chizza, amependekeza kuundwa kwa menejimenti ya muda katika kiwanda cha chai
cha Mponde kama njia ya kusuluhisha mgogoro uliopo kati ya
wakulima wa chai na mwekezaji wa kiwanda hicho, Kampuni ya Chai
Lushoto.
Injinia Christopher
Chizza, katikati.
Akizungumza
katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika
uwanja wa mazoezi katika kata ya Mponde, Chiza pia aliahidi
kushughulikia mgogoro uliopo kati ya wakulima hao wa chai na mwekezaji wa
kiwanda cha chai cha Mponde, kilichopo Bumbuli, mkoani Tanga, ili kiendelee kutoa
huduma bora.
Alisema katika kumaliza mgogoro huo, atazungumza na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda kuhusu suala hilo ili kusaidia kupata ufumbuzi wa kudumu wa mgogoro huo.
Alisema katika kumaliza mgogoro huo, atazungumza na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda kuhusu suala hilo ili kusaidia kupata ufumbuzi wa kudumu wa mgogoro huo.
"Nitaishauri serikali kuchukua
kiwanda hicho na baadaye kuwakabidhi wananchi
ambao ndio wamiliki wa kiwanda hicho,"
alisema.

No comments:
Post a Comment