EBENEZA MARCH 9 2014

EBENEZA MARCH 9 2014

Monday, August 5, 2013

Vuta nikuvute Uchaguzi wa TFF waendelea, Michael Wambura akirusha kombora zito usoni mwa Rais Tenga na Kamati zake



TAARIFA KWA VYOMBO HABARI

YAH:SABABU ZA KUUNGA MKONO UAMUZI WA MSAJILI WA VYAMA VYA MICHEZO NA VILABU KUKATAA KUSAJILI MAREKEBISHO YA  KATIBA  YA TFF KUTOKANA  UKIUKWAJI  WA UTARATIBU NA SHERIA ZA MAREKEBISHO YA KATIBA TFF  2013
Michael Wambura, pichani
Katiba ya TFF ya 2012 ilifutwa na msajIli wa vyama vya michezo na vilabu kwa kuwa ilibadilishwa kinyume cha sheria(BMT)  pamoja na Katiba ya TFF ibara ya 30  kwa kutumia njia ya waraka badala ya Mkutano Mkuu,  hivyo katiba halali kisheria inayotambulika ni ile ya 2006 na mabadiliko yake . FIFA  na Serekali kupitia wizara yenye dhamana na  michezo iliiagiza  TFF iitishe Mkutano Mkuu ili ifanye mabadiliko ya katiba stahiki kwa mujibu wa katiba  na  kwa kufuata taratibu zilivyoainishwa  kwenye katiba ya TFF. Nimelazimika kuendelea kuiunga mkono Serikali kupitia  msajili  kwa maamuzi yake ya kukataa kusajili mabadiliko  ya katiba ya TFF kwa kuwa TFF  kwa makusudi   imeendelea kuvunja katiba yake katika kufanya mabadiliko.
Read more »

January Makamba, Kagasheki waipiga tafu Habari Group kusaidia watoto yatima jijini Dar es Salaam



Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
WANACHAMA wa Kikundi cha Waandishi wa habari wanaojihusisha na ujasiriamali (Habari Group), wametoa msaada wa vyakula na nguo wenye thamani ya sh. milioni moja kwa vituo viwili vya kulelea watoto yatima kwa ajili ya sikukuu ya Idd El Fitri.
January Makamba, Naibu Waziri wa Sayansi na Teknolojia
Msaada huo uliofadhiliwa na wadau mbalimbali ulikabidhiwa juzi, na wanakikundi hao ikiwa ni njia ya kuonyesha ushiriki wao katika masuala ya jamii.
Vituo vilivyokabidhiwa msaada huo ni Kituo cha Kulelea watoto yatima cha Tahfidhil-Qur-An Al-Hidaya kilichopo Buguruni na kituo cha Al Furqaan Islamic kilichopo Chanika.
Read more »

Mkuu wa Mkoa Singida atembelea banda la Wizara ya Uchukuzi, katika maonyesho ya wakulima mjini Dodoma

 Mkuu wa Mkoa wa Singida akiweka sahihi kwenye kitabu cha wageni katika banda la Wizara ya Uchukuzi, wakati alipotembelea mabanda ya Wizara hiyo na Taasisi zake leo mchana katika maonesho ya kitaifa ya kilimo yanayofanyika kitaifa mkoani Dodoma. Kauli Mbiu ya Mwaka huu ni "Zalisha mazao ya kilimo na Mifugo kwa kulenga mahitaji ya Soko'.

Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhe. Dkt. Parseko V. Kone, akimskiliza Afisa Huduma za Abiria wa Mamlaka ya Reli ya Tanzania na Zambia (TAZARA), Bw. Peter Ngwale(wa pili kulia) wakati alipotembelea banda la Mamlaka hiyo  leo mchana, katika maonesho ya Kilimo nanenane yanayofanyika kitaifa katika viwanja vya Nzuguni,Dodoma.

No comments:

Post a Comment