Mkurugenzi wa Kampuni ya kizalendo
ya Kotes (T) Ltd, Max Komba (wapili kulia-waliosimama), akikagua
uchimbaji mtaro kwa ajili ya kutandika nyanya za mfumo wa mawasiliano
kwenye kituo cha Polisi Oysterbay, Dar es Salaam, jana, kuunganisha
kwenye mkongo wa mawasiliano wa taifa. Kulia ni Mhandisi wa masuala ya
ICT, Makao Makuu ya Polisi, Mosses Maganza na watatu ni mhandisi wa
Kotes (T) Ltd, Mohamed Sibuga.
HABARI KAMILI
DAR ES SALAAM, Tanzania
JESHI la Polisi nchini limechukua hatua
za kujiimarisha zaidi katika kuukabili uhalifu kisasa zaidi kwa kuamua
kuviunganisha vituo vyake vikubwa kwenye mtandao wa mawasiliano katika
mkongo wa taifa.
Kufuatia hatua hiyo, ujenzi wa
miundombinu ya mawasiliano hayo ya kuunganishwa kwenye mkongo wa taifa
wa mawasiliano, umeshaanza kwenye vituo vikubwa vya polisi katika mikoa
ya Mwanza, Arusha, Kilimanjaro, Zanzibara na jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na waandishi wa habari,
jana, Mkurugenzi wa Kampuni ya Kotes (T) Limited iliyopewa na jeshi la
polisi kutengeneza mindombinu hiyo, Max Komba, alisema, ujenzi huo
ulianza kwenye Kituo cha Polisi Kurasini, Chuo Cha Polisi Chang'ombe na
Oysterbay ambako ujenzi wake ulitarajiwa kukamilika jana.
Komba alisema, kampuni yake imepewa
kufanya kazi katika mikoa hiyo kwa wiki tatu, tangu ilipoanza Julai 27
mwaka huu kwa mujibu wa mkataba, na ujenzi unatakiwa ume imekamilika
ifikapo Agosti 20 mwaka huu.
Likizungumzia mradi huo, Jeshi la
Polisi kupitia msemaji wake, lilisema, mradi huo ukikamilika utasaidia
jeshi hilo kupunguza gharama na muda mwingi ambao limekuwa likilazimika
kutumia katika kufuatilia kumbukumbu katika kuwatambua wahalifu.
Msemaji wa Jeshi hilo, Advera Senso,
alisema, kupitia mtandao huo, vituo vilivyounganishwa vinaweza kupata
taarifa na kuziona kwa wakati mmoja na kwa haraka zaidi, jambo ambalo
litawezesha kumbaini mhalifu haraka zaidi na kuwa na ushahidi wa kutosha
baada ya kumnasa.
"Mradi huu ni miongoni mwa maboresho
mengi tunayofanya katika jeshi la polisi ili kwenda na wakati. Hivyo
baada ya kukamilisha kwenye vituo vyenye hadhi ya mikoa kipolisi,
tunatarajia pia kushuka hadi ngazi za wilaya kulingana na mahitaji",
alisema.


No comments:
Post a Comment