![](//2.bp.blogspot.com/-7mebLGVK5J4/Ucm5YnBB61I/AAAAAAAAiIU/vM-_ro8-YxU/s1600/4.jpg)
VIJANA watatu wa familia moja ya Felipe Ramirez, wamepata balaa kubwa baada ya kuota matiti yaliyosababisha kuchekwa na vijana wenzao waliokuwa wakiwaona kuwa ni mashoga. Vijana hao kutoka katika Jamhuri ya Dominica ni Yeuri (17 ), Gabriel (11) na Daniu RamÃ
rez (12), hata hivyo, kwa sasa wanaishi kwa amani baada ya kufanyiwa upasuaji na kuondolewa matiti hayo. Baba yao mzazi, Felipe Ramirez alifanya jitihada ya kuomba msaada kupitia televisheni na magazeti ili wanawe wafanyiwe upasuaji kwani walikuwa wakiishi katika mateso kwenye jamii yao. Baada ya kuomba msaada, Mkurugenzi wa Hospitali ya ...
TUPE MAONI YAKOUCHAGUZI WA ARUSHA WAAHIRISHWA TENA ILI KUIMARISHA HALI YA AMANI NA UTULIVU
![](http://2.bp.blogspot.com/-7mebLGVK5J4/Ucm5YnBB61I/AAAAAAAAiIU/vM-_ro8-YxU/s1600/4.jpg)
VIJANA watatu wa familia moja ya Felipe Ramirez, wamepata balaa kubwa baada ya kuota matiti yaliyosababisha kuchekwa na vijana wenzao waliokuwa wakiwaona kuwa ni mashoga. Vijana hao kutoka katika Jamhuri ya Dominica ni Yeuri (17 ), Gabriel (11) na Daniu RamÃ
rez (12), hata hivyo, kwa sasa wanaishi kwa amani baada ya kufanyiwa upasuaji na kuondolewa matiti hayo. Baba yao mzazi, Felipe Ramirez alifanya jitihada ya kuomba msaada kupitia televisheni na magazeti ili wanawe wafanyiwe upasuaji kwani walikuwa wakiishi katika mateso kwenye jamii yao. Baada ya kuomba msaada, Mkurugenzi wa Hospitali ya ...
![](http://4.bp.blogspot.com/-wEZzcwJ6HQc/UcqCNu9KnSI/AAAAAAAAiKo/PLCdbpR3pVw/s1600/jaji.jpg)
TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imeahirisha tena uchaguzi wa madiwani kata nne za Arusha hadi Julai 14 kuruhusu kurejea utulivu baada ya mlipuko wa bomu kwenye mkutano wa kampeni wa Chadema ulioathiri uchaguzi huo wiki iliyopita. Bomu hilo lilirushwa Juni 15 na mtu asiyejulikana katikati ya mkutano wa Chadema katika viwanja vya Soweto, mjini Arusha na kusababisha vifo vya watu watatu na wengine kujeruhiwa na uchaguzi huo wa Juni 16 kulazimika kuahirishwa. Baada ya tukio hilo, Msimamizi wa Uchaguzi wa Arusha aliuahirisha hadi Juni 30, lakini jana Mwenyekiti wa NEC, Jaji Damian Lubuva alisema utafanyika Julai. Kata zinazohusika...
ULINZI WA RAIS OBAMA JIJINI DAR NI BALAA....MITAMBO MBALIMBALI YA MAWASILIANO IMEFUNGWA UWANJA WA NDEGE WA KIA
![](http://2.bp.blogspot.com/-FDx4ZYNrwf4/Ucp-hND9cLI/AAAAAAAAiKY/g3y70kMd8hk/s1600/obama.jpg)
Maandalizi ya ujio wa Rais wa Marekani, Barack Obama nchini yanazidi kupamba moto huku maofisa wa usalama wa Marekani wakipiga kambi katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam. Aidha, kutokana na ujio huo, Serikali imeagiza mashirika yote ya ndege kubadili ratiba zao za safari Julai Mosi, siku ambayo Rais huo atatua nchini. Jana, waandishi wetu walishuhudia pilikapilika za kuimarisha ulinzi katika uwanja huo jambo ambalo uongozi wa uwanja huo jambo wamelieleza kwamba halijawahi kutokea. Ulinzi haujawahi kutokea Mkurugenzi wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere,...
SERIKALI YATOA TAMKO KUHUSU KAULI YA WAZIRI MKUU...YADAI POLISI WANARUHUSIWA KUPIGA NA KUUA KISHERA
![](http://4.bp.blogspot.com/-M0c9SZRvEf0/Ucp580MOEwI/AAAAAAAAiKI/SvHpqQzGfDQ/s1600/1.jpg)
Serikali imetoa tamko bungeni kuhusu mauaji ya raia mikononi mwa polisi ikieleza kuwa sheria ya kanuni ya adhabu inaruhusu kutumia nguvu za kadiri hata kiasi cha kusababisha madhara au kifo. Kauli hiyo imekuja siku chache baada ya Waziri Mkuu, Mizengo Pinda kunukuliwa bungeni akiwataka polisi kuwashughulikia kwa kuwapiga watu wote wanaokaidi kutii sheria. “…Nasema wapigwe tu, maana tumechoka sasa,” alisema Pinda alipojibu maswali ya papo hapo Alhamisi iliyopita. Akisoma tamko hilo bungeni jana, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Pereira Ame Silima alisema kuwa kifungu cha 18(B) na 18(C) cha Sheria...
"TUTAIFUTA CHADEMA ENDAPO ITABAINIKA KUWA WALIRUSHA BOMU LA ARUSHA WENYEWE"....TENDWA
![](http://4.bp.blogspot.com/-LwQUbXvj-e8/UcoD-cTZmMI/AAAAAAAAiJ4/3l2by5FHk7Y/s1600/tendwa.jpg)
Msajili wa Vyama vya Siasa nchini John Tendwa, amedai kuwa ikibainika kuwa CHADEMA ndio waliohusika katika kulipua bomu katika mkutano wao wa 15/06/2013 atakifuta. Tendwa ameyasema hayo alipokuwa akizungumza katika kipindi cha Hot Mix cha East Africa Television akijibu swali la mtangazaji wa kipindi Adrian Stepp kuhusu hatua zitakazochukuliwa... Alipoulizwa kama itathibitika kuwa CCM ndio walihusika kulipua bomu hilo amedai kuwa hawezi kukifuta kwakuwa kwa kufanya hivyo itakuwa ni kufanya mapinduzi ya kalamu. Source :Jamiiforum...
MH. SUGU AMEACHIWA KWA DHAMANA BAADA YA KUKAMATWA NA POLISI
![](http://4.bp.blogspot.com/-3dhxVB7Cuyc/UcnSxbeSEII/AAAAAAAAiJY/sK3EEF1i7HY/s1600/SUGU.jpg)
MBUNGE wa Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi (SUGU) amekamatwa na Jeshi la Polisi Mjini Dodoma na kuachiwa kwa dhamana. Mwandishi wetu akiwa Mjini Dodoma anasema kwamba Mbunge huyo alikamatwa muda mfupi baada ya kutoka katika vikao vya Bunge. Sugu alikamatwa na kupelekwa katika Kituo Kikuu cha Polisi Dodoma na baada ya kuhojiwa aliachiwa kwa dhamana na kutakiwa kuripoti kituoni hapo kesho asubuhi kwa mahojiano mengine. Hata hivyo taarifa za awali za tukio la kukamatwa kwa Mbunge huyo wa Chama Cha Manedeleo na Demokrasia (Chadema) zinadai kwambwa inatokana na kosa la kutoa maneno ya uchochezi, matusi na dhihaka kwa Waziri Mkuu wa Jamhuri...
SUGU AKAMATWA KWA KUMTUSI WAZIRI MKUU
![](http://4.bp.blogspot.com/-iXQ0aWX8Hv8/UcnAyXLPlSI/AAAAAAAAiJI/kCU1RCLXeQg/s1600/SUGU.jpg)
Habari zilizotufikia hivi punde zinadai kuwa Mbunge wa Mbeya mjini Mh Joseph Mbilinyi amekamatwa kwa kile kinachodaiwa ni uchochezi na kumkashifu Waziri Mkuu Mzengo Pinda. Hivi karibuni, Mh. Sugu alidai kuwa Tanzania haijawahi kuwa na waziri mkuu mpumbavu kama Mizengo pinda. Tunaendelea kufuatilia undani wa habari hii: Post yake facebook: ...
RAIS KAGAME AMVAA MTIKILA....ADAI NI MCHOCHEZI NA ASIYEVUMILIKA
![](http://4.bp.blogspot.com/-3puXv-9_VsQ/UcmgeBcnGOI/AAAAAAAAiFY/xqT3vfpfsuQ/s1600/kagame.jpg)
Baada ya Mtikila kutoa waraka unaodai kuwa Rais Kagame amepenyeza wanyarwanda 35,000 ndani ya Tanzania,Kagame amefunguka na kudai kuwa Mtikila ni mchochezi... Hii ni kauli ya Kagame wa Rwanda: -------------------------------------------------------- Kagame has said Mtikila has extreme genocide ideology, similar to what was promoted in Rwanda in 1960s. He said this at a press conference, adding that Mtikila published an article, calling Tutisi snakes, that they don't deserve to live, and showed great hate! The president also said that mtikila tried to regionalize...
PAMOJA NA TISHIO LA USALAMA - KAGAME CUP YAENDELEA HUKO DARFUR - TIMU ZA RWANDA, UGANDA, SUDAN, DJIBOUT NA BURUNDI ZASHIRIKI I
Mashabiki wakiwa uwanjani kuangalia mojawapo ya mtanange wa CECAFA Kagame Cup |
Jumatano wiki hii Express ya Uganda inapimana nguvu na APR ya Rwanda kisha wenyeji Al Ahly Shandy dhidi ya Al Merreikh ya kutoka El Fashir, mji mdogo ambao una uwanja wa kimataifa wa ndege pamoja na viwanja vya kisasa vya voliboli, mpira wa kikapu na kandanda.
Mechi hiyo ya wenyeji inasubiriwa kwa hamu. Al Merreikh ina mashabiki wengi na wachezaji kadhaa wa nje baadhi yao Joseph Kabagambe ambaye ni mchezaji kutoka Uganda wa kiungo cha kati na Adam Williams wa Nigeria. Mchezaji mwingine wa Nigeria David Nwosu anayechezea Merreikh hatacheza kwa sababu ya kuonyeshwa kadi mbili za manjano..
Kabla ya mechi jioni ya saa 10 mashabiki wanapata nafasi ya kushiriki swala ya Alsir |
Alhamisi wiki hii Vital'O ya Burundi inapepetana na Ports ya Djibouti mechi ya kwanza ya robo-fainali, na ya pili ni kati ya Rayon ya Rwanda na URA ya Uganda. Mechi za nusu-fainali ni Ijumaa na Jumamosi kisha Julai tarehe mosi ni mechi ya fainali.
BAADA YA KUSHINDWA KUIPELEKA CONGO BRAZIL 2014 - KOCHA LEROY AJIUZULU
Claude LeRoy ameachia ngazi kama kocha wa timu ya taifa ya Jamuhuri ya kidemokrasia ya Congo.
Kocha huyo kutoka Ufaransa mwenye umri wa miaka 65 alichukua wadhifa huo wa kuifundisha timu ya Congo kwa mara ya pili mwezi Septemba mwaka 2011."Niliwambia wachezaji wangu kwamba nitaachia ngazi baada ya miaka miwili," alisema Le Roy, ambaye mechi yake ya mwisho ilichezwa jumapili iliyopita dhidi ya Cameroon. Timu mbili zilitoka sare ya bila kufungana, katika mechi za mchujo wa kutafuta tiketi ya fainali za kombe la dunia.
Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo DR Congo haitafuzu katika fainali za kombe la dunia nchini Brazil mwaka 2014 na kama ilivyotarajiwa Timu ya taifa ya Cameroon ilipewa alama tatu baada ya Togo kukiri kwamba mapema mwezi huu ilimtumia mchezaji ambaye hakuruhusiwa kucheza.
LeRoy alisaidia Jamuhuri ya kidemokrasia ya Congo kufuzu kwenye fainali za kombe la mataifa ya bara la Afrika mwaka 2013 nchini Afrika kusini, lakini ikashindwa kuvuka hatua ya makundi licha ya kutopoteza mechi hata moja.
Ni kwa mara ya saba LeRoy akisaidia timu kufuzu kwenye fainali za kombe la Afrika baada mafanikio yake akiifundisha Cameroon na kunyakua kombe hilo mwaka 1988. Pia alizifundisha Senegal na Ghana.
MKATABA MNONO WA CHELSEA NA ADIDAS WAMPA MOURINHO MSULI WA KUPAMBANA KWENYE SOKO LA USAJILI BILA KUHOFIA 'FINANCIAL FAIR PLAY'
JOSE MOURINHO amewashiwa taa ya kijani ya kuanza kufanya balaa kwenye usajili baada ya Cheslea kusaini mkataba mnono wa £300million na kampuni ya utengenezaji wa mavazi ya kawaida na kimichezo ya adidas.
Mkataba wa miaka 10 baina ya Chelsea na Adidas ndio unaoshika nafasi ya kwanza kwa thamani baina ya klabu na kampuni ya utengenezaji jezi za klabu husika.Mkataba huo umeondoa wasiwasi wa Chelsea kuvunja sheria za Financial Fair Play.
Dili hilo la Chelsea na Adidas limevunja rekodi ya dili la Manchester United na Nike lilokuwa na thamani ya £287m ambalo lilisainiwa miaka 13 iliyopita na linaisha mwaka 2015.
Mkataba unamaanisha Chelsea hawatokuwa wakimtegemea zaidi Abramovich kuvunja benki katika kuiwezesha timu hiyo.
Mkataba uliopita na Adidas ulisainiwa mwaka 2006 ulikuwa na thamani ya £20million kwa mwaka.
LIVERPOOL WAENDELEZA VURUGU KWENYE USAJILI: WAKAMILISHA USAJILI WA MCHEZAJI WA NNE - GOLIKIPA MIGNOLET WA SUNDERLAND
Liverpool wamekamilisha usajili wa nne katika dirisha hili la usajili baada ya kutangaza kukamilisha usajili wa golikipa Simon Mignolet kutoka Sunderland kwa ada ya uhamisho ya £9million.
Golikipa huyo amekuwa akitamaniwa na Brandan Brendan Rodgers kwa muda mrefu, na sasa anatajwa kuja kuchukua nafasi ya kwanza kwenye kikosi cha Liverpool mbele ya Pepe Reina.
Golikipa huyo amekuwa akitamaniwa na Brandan Brendan Rodgers kwa muda mrefu, na sasa anatajwa kuja kuchukua nafasi ya kwanza kwenye kikosi cha Liverpool mbele ya Pepe Reina.
ANDRE SCHURRLE - MCHEZAJI WA KWANZA KUSAJILIWA NA MOURINHO CHELSEA MSIMU HUU - ANGALIA UWEZO WAKE
Jose Mourinho amefungua rasmi akaunti ya Chelsea na kukamilisha usajili wa mshambuliaji wa kijerumani ANDRE SCHURRLE - ambaye leo hii amefaulu vipimo vya afya na kujiunga rasmi na Chelsea akitokea Bayern Leverkusen.
Chelsea wamempa mjerumani huyo mkataba wa miaka mitano, na kuwa mchezaji wa kwanza kusajiliwa na Jose Mourinho tangu arejee kutoka Santiago Bernabeu mapema mwezi uliopita.Schurrle, 22, alisema: “Nina furaha kusajili hapa. Ni heshima kubwa kwangu kuichezea klabu hii, ninaangalia mbele kuitumikia timu hii.”
Schurrle ana uwezo wa kucheza aidha kama winga au mshambuliaji wa kati akiungana na wachezaji wengine kama Juan Mata, Eden Hazard, Oscar na Kevin De Bruyne katika kugombea nafasi ya kuwemo katika kikosi cha kwanza cha Mourinho.
Schurrle amepewa jezi namba 14.
ANGALIA MAVITU YAKE KWENYE VIDEO HII HAPA CHINI
ETHIOPIA WANYANG'ANYWA POINTI NA KUWEKA REHANI NAFASI YA KUFUZU KOMBE LA DUNIA - KATIBU MKUU WA SHIRIKISHO ATIMULIWA
Shirikisho la soka nchini Ethiopia limemfukuza kazi katibu mkuu wake siku ya jumatatu baada ya taifa hilo kukumbwa na skendo iliyothibitishwa ya kuchezesha mchezaji asiyestahili kwenye mechi ya za mashindano ya kufuzu kombe la dunia, kosa ambalo limewagharimu kukatwa pointi 3.
Shirikisho hilo lilifanya mkutano na kupiga kura ya kumtimua Ashenafi Ejigu lakini wakaikataa barua ya kujiuzulu ya makamu wa raisi wa shirikisho hilo Berhanu Kebede, ambaye huko nyuma nae aliingizwa kwenye mkenge wa lawama.
Baadhi ya wajumbe wa shirikisho na waandishi waliokuwepo kwenye mkutano huo walitaka uongozi mzima wa shirikisho hilo uondolewe.
Sahilu Gebremariam, Raisi wa shirikisho hilo, alisema kwamba alikuwa anajiandaa kutuma barua ya kujiuzulu katika uchaguzi ujao wa kugombea siti katika kamati kuu ya shirikisho hilo.
"Hili ni kosa kubwa kutokea kwenye soka, hivyo inabidi viongozi wote tuwajibike kwa makosa haya kwa kujiuzulu," Sahilu aliiambia Reuters. "Lakini tuna majukumu mengine mbele yetu hivyo ikaamuriwa tubaki mpaka September."
Ushindi wa Ethiopia wa 2-1 dhidi ya South Africa jijini Addis Ababa katika mechi ya June 16 uliwapa Ethiopia uongozi wa pointi 5 kwenye kundi lao ambazo zisingeweza kufikiwa na timu yoyote hivyo wakawa wamefuzu rasmi kwenda kwenye hatua ya mtoano kwa ajili ya kufuzu kwenda michuano ya kombe la dunia 2014 nchini Brazil.
Lakini masaa kadhaa baadae, FIFA ikasema kwamba inachunguza tuhuma za Ethiopia kumchezesha mchezaji ambaye alikuwa kasimamishwa - kiungo Minyahile Beyene ambaye alicheza kwenye mechi dhidi ya Botswana June 8.
Minyahile alikuwa na kadi mbili za njano katika mechi zilizopita za kufuzu, na sheria za World Cup zinasema kwamba mchezaji ambaye amepewa kadi mbili za njano kwenye mechi zilizopita za kufuzu anapaswa kutokucheza mechi moja inayofuatia.
Alionyeshwa kadi ya njano kwenye mchezo wa sare ya 1-1 dhidi ya South Africa mwaka mmoja uliopita na mara nyingine alionyeshwa kwenye mechi ya ushindi wa 1-0 dhidi ya Botswana mwezi March mwaka huu.
Ethiopia, ambao hawajawahi kufuzu fainali za kombe la dunia, wanategemewa kunyang'anywa pointi 3 hivyo kumaanisha kwamba nafasi ya kusonga mbele kwenye kundi lao (A) sasa imebaki wazi.
Maofisa wa Ethiopia walisema kwamba walikosea kumchezesha mchezaji kwa bahati mbaya. Makamu wa Raisi wa shirikisho Berhanu, ambaye pia alikuwa kiongozi wa timu wakati wa mechi dhidi ya Botswana, alisema kwamba walipoteza barua ya FIFAya kuwataarifu kuhusu kadi za Minyahile.
Ikiwa Ethiopia watanyang'anywa pointi 3 basi watabakia na pointi 10, huku South Africa wakiwa na 8, na Botswana wakiwa 7 - huku kila timu ikiwa na mchezo mmoja mkononi.
Ethiopia watacheza mechi yao ya mwisho na Jamhuri ya Afrika ya Kati mwezi wa tisa tarehe 6, wakati South Africa watatimbana na Botswana.

WABUNGE WAFANYA JOGING MKOANI DODOMA
Mbunge wa Kinondoni, Idd Azan akiwapanga washiriki wa Joging katika Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Hawa Ghasia wa pili kutoka (Kulia), Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Amos Makalla wa pili kutoka (kushoto), Mbunge wa Iramba Magharibi, Mwigulu Nchemba (kulia) na Mbunge wa Kinondoni Idd Azan (kushoto) wakiongoza mazoezi ya kukimbia ya Kilomita kumi yaliyoanzia katika Uwanja wa Jamhuri na kushirikisha baadhi ya wabunge, timu ya Barafu Joging ya Dar es Salaam na Muungano ya mkoani Dodoma.
Hawa Ghasia na Idd Azan wakishiriki Joging mkoani Dodoma leo
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiw6MhDFnqNbdo9L_Ta0L-CfsqVTakcsDEDMWoDom70KouXtO0uc72cUFmBpdkKkL5TLdEfcAtkdtbGttGe3z2hqEj3dG6JuZ2HRiV3E_KwSRVrcs7sxSX9KtDWB1XepIDMiUISIT7ecic/s640/IMG_1966.jpg)
washiriki wa Joging timu ya muungano kutoka mkoani Dodoma na timu ya Barafu Joging Sports Club ya jijini Dar es Salaam wakiwa pamoja na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Hawa Ghasia
washiriki wa Joging wakifanya mazoezi ya viungo baada ya kumaliza mbio za kilomita kumi
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgeWtMSujRTVhm83Dyaii-YoCaE3hBIELt8KPRfqTEGy1zSOtILYRxqw8aWkB_evP6-CggVRah6tTwkICpSCpJQ7gtrb5F5B3y57AE2sT0eO8CsOGB295rH1ABgwa1K_v-IUR5MW08xjQE/s640/IMG_1984.jpg)
Hawa Ghasia akiwa na timu ya Joging ya Barafu Sports Club na Muungano
Kulia ni Mbunge wa Nzega Dk. Khamis Kigwangala akishiriki mazoezi ya viungo baada ya kumaliza mbio za kilomita kumi
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Hawa Ghasia akishiriki mazoezi ya viungo
Mbunge wa Namtumbo, Vita Kawawa akishiriki Joging katika Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma
WANASOKA MAARUFU NCHINI WAHITIMU KOZI YA UKOCHA YA NGAZI YA KATI LEO.
Picha ya pamoja kati wa wahitimu wa kozi ya ukocha ngazi ya kati na Viongozi wa TFF na DRFA.
Kutoka kushoto: Omary Mbarouk Omari,Ibrahim Masoud 'Maestro',Rechel Palangyo na Moses Mkandawile. Nahodha wa zamani wa Simba Sc, Selemani Matola akipewa mkono wa pongezi na Rais wa TFF ndugu Leodegar Tenga Kutoka kushoto: Selemani Matola,Rechel,Zubeir Katwila na Steven Nyenge.
Kutoka Kushoto: Mwenyekiti wa DRFA,Almasi Kasongo,Rais wa TFF Leodegar Tenga,Mkurugenzi wa Ufundi wa TFF ndugu Sunday Kayuni na mwakilishi wa TAFCA
Mimi pia nilikuwa miongoni mwa wahitimu wa kozi hiyo ya ukocha.
Golikipa wa zamani wa Simba Sc na Taifa Stars Moses Mkandawile akipeana mkono wa pongezi na Bwana Tenga.

BREAKING NEWS: CARLO ANCELOTTI ATHIBITISHWA KUWA KOCHA MPYA WA MADRID - BEKI WA ZAMANI WA MAN UNITED ARITHI KIBARUA CHAKE PSG
Hatimaye Real Madrid wamemtangaza kocha Carlo Ancelotti kuwa kocha wao mpya.
Kocha huyo wa zamani wa Chelsea na PSG amechukua nafasi iliyoachwa wazi na na Jose Mourinho, ambaye amerudi Stamford Bridge.
Ancelotti, 54, amesaini mkataba wa miaka mitatu kuongoza benchi la ufundi la Santiago Bernabeu
Wakati akiondoka PSG, mchezaji wa zamani wa kimataifa wa Ufaransa na beki wa Manchester United Laurent Blanc ameteuliwa kuchukua nafasi ya Ancelotti ndani ya klabu hiyo inayomilikiwa na waarbu matajiri kutoka Qatar.

Blanc tayari ana uzoefu na kazi ya ukocha baada ya kuzifundisha klabu ya Bordeaux na timu ya taifa ya Ufaransa.
KALI YA LEO: MANCHESTER CITY YAPIGA MARUFUKU WAFANYAKAZI WAKE KUVAA JEZI ZA MAN UNITED - WAKIWA KAZINI.
Manchester City wamewapiga marufuku wafanyakazi wake kuvaa jezi za Manchester United wakati wakiwa kazini.
The Mirror inaripoti kwamba wafanyakazi wanaofanya kazi ya ujenzi wa kituo kipya cha kambi ya Man City - Etihad chenye thamani ya £120million wameonywa kwamba watafuuzwa ikiwa watakuja kazini wakiwa kwenye uzi mwekundu wa United.
Kwa mujibu wa mfanyakazi mmoja anayefanya kazi kwenye eneo hilo la ujenzi amesema jezi za timu nyingine zote zimepigwa marufuku kuonekana zimevaliwa kwenye eneo hilo ambalo litakuwa na uwanja mpya wa mazoezi wa City.
Hatua hii imekuja baada ya tukio lilotokea wiki iliyopita ambapo wajenzi wawili wapenzi wa United walikwenda site wakiwa wamevalia jezi za United na hivyo wakaambiwa wavue jezi ndio waendelee na kazi.

No comments:
Post a Comment