"TUKIO LA ARUSHA LIMENIFANYA NIAMINI KUWA TANZANIA KUNA WANARIADHA WAZURI".....HUU NI UTUMBO WA MBUNGE SERUKAMBA
![](http://3.bp.blogspot.com/-nKYy95SluM4/UcJiKBExypI/AAAAAAAAh4A/D02YstB2RyQ/s1600/S.jpg)
Tukio la bomu la Arusha limewasitua wengi kufuatia vifo vya
wananchi wanne wasio na hatia....
Nasema hawana hatia kwa sababu siku ya tukio wananchi hao
walikuwa katika mkutano wa hadhara wa chama chao ( CHADEMA ) sawa
na ambavyo wangeweza kuwa katika mkutano mwingine wowote wa
kisiasa....
Pamoja na majonzi waliyonayo wananchi, wanasiasa wetu wanaonekana
kutoguswa kabisa na vifo hivyo ...
"NASSARI NI MUONGO NA NI MNAFIKI, TUMEMRUHUSU KWA AMANI NA BADALA YAKE KADAI ETI KATOROKA ILI TUSIMUUE"...KAULI YA DAKTARI
![](http://4.bp.blogspot.com/-JxqpRh_98w0/UcJVCsoe7PI/AAAAAAAAh3Q/V9gODfQ-Cvc/s1600/2.jpg)
UONGOZI wa hospitali ya Kanisa la Kiinjili
la Kilutheri Tanzania (KKKT) ya Selian jijini Arusha umekanusha vikali
taarifa zilizotolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Chadema John
Mnyika kuwa serikali ilipeleka maafisa wa usalama hospitalini hapo kwa
lengo la kumdhuru mbunge wa jimbo la Arumeru Mashariki Joshua Nassari
pamoja na majeruhi wa mabomu waliolazwa katika hospitali hiyo na kusema
ni uzushi mtupu.
Mnyika alisema
kufuatia kitendo hicho mbunge Nassari alipiga kelele (yowe) akiwa
katika korido ya wodi namba 14 aliyokua amelazwa ili kuomba msaada
baada ya maafisa hao wa usalama waliokua wamevalia mavazi ya kitabibu
na...
VIONGOZI WA CHADEMA NA WANANCHI WA ARUSHA WAMEACHIWA KWA DHAMANA.....POLISI YAMTAKA MBOWE APELEKE USHAHIDI KWA RAIS KIKWETE
![](http://1.bp.blogspot.com/-ykFYrrikxPQ/UcIOFlT9wCI/AAAAAAAAh3A/7Y4nTfpHZ_k/s1600/1.jpg)
Jeshi la polisi nchini limewaachilia kwa dhamana viongozi wa Chadema na
wananchi wote waliokuwa wanashikiliwa na limemtaka mwenyekiti wa Chadema
Mh. Freeman Mbowe kuwasilisha ushahidi wa mtu aliyelipua bomu kwenye
mkutano kwa Mh. Rais kama hana imani na jeshi la polisi.
(VIDEO: ITV)...
IDD SIMBA NA WENZAKE WAACHIWA HURU KATIKA KESI YA KUHUJUMU UCHUMI
![](http://1.bp.blogspot.com/-YFDhNGOBjGI/UcILW5TIjhI/AAAAAAAAh2o/Nb5aMJ6Uwh8/s1600/1.jpg)
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam leo hii imemwachiria huru
Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Usafiri Dar es Salaam (UDA), Idd Simba
pamoja na Mkurugenzi wa Bodi hiyo ambaye alikuwa Diwani wa Kata Sinza
(CCM), Salum Mwaking’inda vile vile Meneja Mkuu wa shirika hilo Victor
Milanzi na Mkurugenzi wa Kampuni ya Simon Group , Simon Kisena waliokuwa
wakikabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi wa shirika hilo.Mahakama
imewaachia huru washitakiwa kwa sababu Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP),
Dk Eliezer Feleshi alliwasilisha hati ya kutokuwa na haja ya kuendelea
kuwashitaki washitakiwa hao chini ya kifungu cha 91(1) cha Sheria ya
Mwenendo...
JOHN MNYINKA ADAI KUWA KESHO WATAWASHA MOTO TENA JIJINI ARUSHA
![](http://3.bp.blogspot.com/-rwMvDgdRzTA/UcIIUMbQS9I/AAAAAAAAh2Q/AM2pm_ZSnSY/s1600/2.jpg)
WAKATI Jeshi la Polisi Mkoani Arusha ikiendelea kumsaka Mwenyekiti wa
Chadema Freeman Mbowe na Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini Godbless
Lema,Mbunge wa Ubungo John Mnyika kesho atawasha moto mwingine wa
maombolezo uliotawanywa kwa mabomu jana.
Mnyika atakuwa msatari wa mbele kuongoza wafuasi wa Chadema kuaga
miili ya watu watatu waliouawa katika shambulio la kigaidi Jumamosi
iliyopita kwenye Uwanja wa Soweto.
Mbali na Mnyika zoezi hilo pia litasimamiwa na wabunge wanne wa
Chadema walioachiwa huru kwa dhamana leo kwakua upelelezi wa kesi zao
hazijakamilika.
wabunge hao waliachiwa huru kwa dhamana katika Kituo Kikuu cha...
SERIKALI YA MAPINDUZI ZANZIBAR YATOA SALAMU ZA RAMBIRAMBI KWA MKUU WA MKA WA ARUSHA
![](http://1.bp.blogspot.com/-3le1vXzwsb0/UcG8jROG6KI/AAAAAAAAh1g/6N_W5oJ52ZM/s1600/ZNZ.jpg)
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar
imetuma salamu za rambi mbali kwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mh. Magesa
Muhongo kutokana na vifo vya wananchi watatu wa Mkoa huo vilivyotokea
kufuatia mripuko wa bomu uliotokea juzi katika viwanja vya Soweto Jijini
Arusha.
Watu
wasiopungua 70 waliripotiwa kujeruhiwa wakati wa mripuko huo kwenye
mkutano wa hadhara wa kampeni za uchaguzi katika Kata ya Soweto wa Chama
cha Demokrasia ya Maendeleo { Chadema }.
Katika
Taarifa ya rambi rambi ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar iliyotumwa
kwa Mkuu huyo wa Mkoa wa Arusha na kutiwa saini na Makamu wa Pili wa
Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alielezea...
VIDEO NYINGINE YA VURUGU ZA ARUSHA IKIONESHA JINSI WATU WALIVYOPOTEZA MAISHA
![](http://3.bp.blogspot.com/-U6fl2OquTFg/UcG2kt-KwqI/AAAAAAAAh1A/2rix7uf-qds/s1600/1.jpg)
VIDEO NYINGINE YA VURUGU ZA ARUSHA IKIONESHA JINSI WATU WALIVYOPOTEZA
MAISHA
...
No comments:
Post a Comment