Miaka
12 iliyopita, klabu ya Argentina San Lorenzo ilikuwa ikihitaji ushindi
katika mchezo wa mwisho wa ligi ili kushinda ubingwa wa nchi hiyo.
Manuel Pellegrini, kocha wa timu hiyo aliutumia usiku wa siku ya kuamkia
mechi akisoma kitabu kwenye chumba kimojawapo kwenye kambi ya klabu
hiyo. Umakini wake kwenye kusoma kitabu ulikatishwa, Fabricio Coloccini,
wakati huo akiwa na miaka 19 akiichezea timu hiyo kwa mkopo, alikuwa
akitoka chumbanikwake na kutembea kwenye korido, akionekana mwenye
mawazo na hivyo kushindwa kulala, pia alikuwa na wasiwasi hata
akashindwa kukaa chini akabaki anatembea tembea tu.
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEh-PuSjyF9sx91lvfMvlZLnCRN51YTKFSnKiVeaBvMpGGnBjTYyd4SI_4XBWCo3XQHtRGWLHieheWxaL8JGImZKTc2BtUAlny-DDjsY9NIoE41YQoocDuG2jnoLApOPtUGelPlEATGqasc/s640/colocha.jpg) |
Coloccini akiwa na wachezaji wa San Lorenzo wakishangilia |
Pellegrini
akuweza kuinuka kutoka alipokaa kwenda kumtuliza mlinzi huyo wa
kiargentina bali alimwambia: "Fabricio, acha kuwa na wasiwasi kuhusu
kitu chochote. Tumeshajitahidi na kufanya vizuri msimu wote, hivyo
haitokuwa jambo kubwa sana kama tukichukua kombe au tusichukue."
"Unamaanisha
nini?" Coloccini aliuliza. "Namaanisha kwamba - timu yetu ni bora
kuliko zote, hilo ndio jambo muhimu, hivyo sijali kama tutashinda au
kufungwa kesho."
Coloccini hakuweza kuamini maneno aliyokuwa
akiyasikia kutoka kwa kocha wake. Alishangazwa sana na kauli za mwalimu
wake kiasi akashindwa hata kujibu, alirudi chumbani kwake na kulala.
Siku iliyofuatia wakaenda uwanjani na wakashinda mechi kisha kubeba
ubingwa - na hapo ndipo Coloccini alipoona namna maneno ya Pellegrini
yalivyomtuliza na kumfanya kucheza bila wasiwasi na matokeo kuisadia
timu yake kubeba ubingwa. Kuna makinda wengi katika kikosi cha
manchester City ambao watakuwa chini ya Pellegrini baada yaMuargentina
huyo kutua Etihad - ambao watafaidi matunda ya falsafa ya saikolojia za
kocha huyu.
Mapema
mwezi huu, Pellegrini aliwahutubia makocha takribani 900 katika
mkutano wa kimataifa wa makocha uliofanyika Malaga - Spain. Aliongolea
mbinu anazotumia zilizomfanya aweze kuifikisha Malaga katika robo
fainali ya Champions League msimu uliopita -- kwa bahati mbaya dakika
mbili za nyongeza ziliinyima timu yake nafasi ya kwenda kucheza nusu
fainali baada ya kufungwa walioinga fainali.
KUHUSU FALSAFA ZAKE
"Kuna
vitu vitatu muhimu ninavyohitaji kutoka wachezaji wangu; heshima,
kujitolea/kujituma na kiwango kizuri," aliiambia Diario Sur. "Nina imani
kwamba nitaweza kuingiza staili yangu ya soka katika nchi ya tano
ambayo nitakuwa nafundisha soka ndani yake."
Pellegrini alianza
maisha yake ya soka kwa kuichezea klabu ya Universidad de Chile, ambapo
ilionekana wazi kwamba ujuzi wake wa kuwasoma na kuwaelewa watu
utampeleka mbali. Alikuwa ndio mchezaji pekee aliyekuwa akisoma chuo
kikuu -- alikuwa akichua engineering at Universidad Catolica -- na
alikuwa mmoja kati ya wachezaji maarufu sana katika kikosi cha timu yao.
"Alikuwa
mwanafunzi wa daraja la juu," anakumbuka mchezaji mwenzie Jorge Luis
Ghiso, "lakini kila mtu alimheshimu na kumpenda." aliweza kuwafanya
wakufunzi wake wamruhusu kuondoka darasani dakika 15 kabla ya muda ili
asiwe anachelewa vipindi vya mazoezi.
Pellegrini ni mtu anayeenda
na muda sana. Wakati alipotajwa kuwa kocha wa klabu ya Ecuador Liga
Deportiva Universitaria de Quito, wachezaji wengi wenye makubwa
walichelewa kufika mapema kwenye mchezo wa kirafiki dhidi ya timu moja
ya mtaani - Pellegrini akawafungia mlango katika chumba cha kubadilishia
nguo na kisha kukataa kuwaruhusu kucheza. Hawakuwahi kuchelewa tena sio
mazoezini wala kwenye mechi. Ikiwa kocha aliyepita wa City Roberto
Mancini aliiongoza timu hiyo kwa ubabe kwa wachezaji wake, Pellegrini
anapendelea kuongoza kwa heshima kutoka anaowaongoza.
"Inabidi
uonyeshe kwamba una mamlaka ya kuwa kocha, lakini naweza kuwa dikteta
na pia mwana demokrasia" alisema. "Dikteta kwa sababu wachezaji
wanapaswa kukuheshimu, lakini kidemokrasia kwa sababu inabidi
niwashawishi kama nahitaji wao wafanye hivyo."
City walisema
sababu nyuma ya kufukuzwa kwa Mancini zilikuwa ni kushindwa kupata
mafanikio waliojipangia (ukiachana na kufuzu kwa Champions League) na
pia katika kauli hiyo hiyo walisema wanahitaji kuboresha kwa ujumla
maendeleo ya klabu.
CEO wa zamani wa City Garry Cook aliiambia
BBC kwamba maboresho yaliyohitajika hasa kutoka kwa mwalimu ni - uelewa
mkubwa za meneja kuifanya timu kuwa mali ya umma...kujieleza mbele ya
vyombo vya habari...kuendesha biashara kwa kuwa na management nzuri
katika masuala ya fedha katika kila wanachokifanya. Kwa ujumla ni
kuelewa namna soka la kisasa linavyotaka kuendeshwa kibiashara, na sio
timu kushinda tu mechi."
Uteuzi wa Pellegrini ni uamuzi mwingine
muhimu uliofanywa na viongozi wapya wa kihispaniola - kama walivyoamua
kuwekeza kwenye soka la Marekani kwa kuunda New York City FC, klabu
mpya MLS iliyoundwa kwa kushirikiana na New York Yankees, ni uamuzi
unaoweza kuipeleka City hatua nyingine katika mahitaji yao ya kuteka
soka la ulaya na kupata umaarufu mkubwa duniani kote.
Pellegrini,
ambaye ni msomi mzuri sana hata kwenye mambo ya biashara na masoko ndio
mtu sahihi wa kuitoa City ilipo kwenda hatua nyingine. Tabia yake ya
kujisomea vitabu mbalimbali huwa inamsaidia katika maarifa ya ndani na
nje ya uwanja. Kitabu ambacho alikuwa anasoma wakati Coloccini
anahangaika na kushindwa kulala kule Argentina - kilikuwa kinahusu ni
namna gani mtu au taasisi inaweza kuendelea kwenye masoko.
No comments:
Post a Comment