WANAFUNZI AFRICA KUSINI WAONGOZA KWA VVU
Waziri wa afya wa Afrika Kusini Amesema kuwa zaidi ya
asili mia 28% ya wasichana wa shule wameambukizwa virusi vya Ukimwi,
ikilinganishwa na asili mia 4% tu ya vijana wa shule.
Hii ameelezea ni kutokana pakubwa na kuongezeka
kwa mababa sukari au kwa jina lingine, *fataki*, ( Wazee wanao tembea na
wasichana wadogo kwa umri).
Waziri
Aaron Motsoaledi amesema kuwa wamepata ushahidi kuwa wasichana wengi
wamejiingiza katika mapenzi na wazee waliowazidi ki umri badala ya kuwa
na vijana wa rika lao.
Takwimu za punde zaidi zimeonyesha kuwa asili
mia kumi ya raia wa Afrika Kusini wanaishi na virusi vya HIV. Nchi hiyo
imekuwa na mradi wa kuvuma zaidi wa kutoa dawa za kukabili makali ya
virusi hivyo vya HIV , ARV tangu rais Jacob Zuma alipomteua bwana
Motsoaledi kuongoza wizara hiyo ya afya yapata miaka minee iliyopita.
'Kupotosha watoto'
Waziri huyo pia aliongeza kuwa zaidi ya
wasichana 94,000 walipata mimba katika mwaka wa 2001 and kati yao 77,
000 walilazimika kuavya mimba hizo katika kliniki za serikali, kwa
mujibu wa taarfa katika magazeti ya Soweto.
Akizungumza katika mkutano wa hadhara katika mji
wa Carolina, mkoa wa Mpumalanga, bwana Motsoaledi alisema kuwa idadi
hiyo kubwa ya wasichana wanaoharibiwa maisha yao ''inanivunja moyo
sana''.
''Lazima tuchukue hatua dhidi ya mababa sukari hawa kwasababu wanaangamiza vizazi vyetu''.
Mwaka uliopita zaidi ya watu 260,000 wanaoishi
na Ukimwi walifariki ikiwa ni takriban nusu ya watu wote waliofariki
katika nchi hiyo
No comments:
Post a Comment