EBENEZA MARCH 9 2014

EBENEZA MARCH 9 2014

Friday, October 28, 2016

BARCELONA YAMBURUZA RAIS WA LA LIGA MAHAKAMANI!

KLABU ya Barcelona ya huko Spain, katika hatua ya kushangaza, imempeleka Rais wa La Liga Javier Tebas Mahakamani wakilalamikia kauli zake kufuatia Mechi yao waliyoshinda kwa mbinde 3-2 dhidi ya Valencia.
Kwenye Mechi hiyo iliyochezwa Wikiendi iliyopita, Valencia walipigwa Faini EURO 1,500 baada ya Chupa ya Maji kurushwa toka Jukwaani kwa Washabiki na kuwalenga Wachezaji Uwanjani.
Mbali ya kushushwa Faini hiyo, Kamati ya Nidhamu ya La Liga iliponda vitendo vya Wachezaji wa Barcelona waliposhangilia Bao lao la ushindi la Penati ya Dakika za Majeruhi iliyofungwa na Lionel Messi.

 Akiongea baada ya Mechi hiyo, Rais wa La Liga, Javier Tebas, aligusia ushangiliaji wa Wachezaji wa Barca: “Kitu kikubwa ni ile kurushwa Chupa ya Maji lakini baadhi ya Wachezaji walifanya vitendo ambavyo hatupendi!”
Kauli hiyo imewafanya Barcelona kumburuza Rais huyo kwenye Mahakama ya Michezo na Rais wa Barcelona, Josep Maria Bartomeu, ameeleza: “Kuongelea kuhusu Wachezaji kunachochea zaidi hali tete ambayo inabidi itulizwe. Matamshi ya Tebas ni ovyo na hayastahili kutoka kwa Kiongozi wa Michezo!”
LA LIGA
Ratiba:
**Saa za Bongo
Ijumaa Oktoba 28
2145 CD Leganes v Real Sociedad
Jumamosi Oktoba 29
1400 Sporting Gijon v Sevilla FC
1715 Deportivo Alaves v Real Madrid CF
1930 Atletico de Madrid v Malaga CF
2145 FC Barcelona v Granada CF
Jumapili Oktobo 30
1400 SD Eibar v Villarreal CF
1815 Athletic de Bilbao v Osasuna
2030 Real Betis v RCD Espanyol
2245 Las Palmas v Celta de Vigo
Jumapili Oktoba 30
2245 Deportivo La Coruna v Valencia C.F

No comments:

Post a Comment