EBENEZA MARCH 9 2014

EBENEZA MARCH 9 2014

Friday, May 23, 2014

MOYES AHOJIWA KWA KUMTWANGA SHABIKI ALIYEMLETEA MASHARA



Kocha aliyetimuliwa Manchester United, David Moyes amehojiwa kutokana na kitendo chake cha kumkaba kijana mmoja nje ya baa.
Moyes, 51, alimkaba kijana huyo baada ya kumfanyia mzaha na dharau wakati akiwa na rafiki zake.

Kijana huyo alimuonyesha dharau, hali iliyomuudhi Moyes na moja kwa moja akamfuata na kumkaba moja kwa moja.
Kutokana na dharau hizo, Moyes aligeuka ghafla na kumvaa kijana huyo aitwaye Joshua Gillibrand, 23, akamkaba na kumgonga ukutani.
KIJANA ALIYEKUTANA NA DHORUBA YA MOYES

HII NDIYO BAA TUKIO LILIPOTOKEA.

Gillibrand, amesema alifikiri ndiyo mwisho wa uhai wake kwa kuwa Moyes alimkaba hadi akashindwa kupumua.
“Alinikaba halafu akanipiga ukutani na kuachia, nikaanguka chini na kugonga uso wangu,” Gillibrand aliliambia gazeti la The Sun.
taarifa zinasema, Gillibrand, alifika hospitali akiwa anatokwa damu puani na tayari jeshi la polisi limeeleza nia kuwa limeanza uchungzi wa suala hilo.

No comments:

Post a Comment