EBENEZA MARCH 9 2014

EBENEZA MARCH 9 2014

Monday, April 14, 2014

SHIRIKISHO la mpira wa Kikapu Tanzania(TBF),limesema kukosa kwa kuthaminika kwa mchezo huo hapa nchini, ndio chanzo kikuu cha kukosa wadhamini katika Mashindano yao.

NA MSHAMU NGOJWIKE,
TBF sasa linaendesha Mashindano ya Klabu bingwa ambayo ilianza kunguruma toka Aprili 5 hadi 13 mwaka huu kwenye uwanja wa ndani wa taifa,ikishirikisha timu 24.
Akizungumza na BINGWA jana,Mwenyekiti wa kamati ya  mashindano ya Shirikisho la Mpira wa Kikapu Tanzania(TBF), Michael Mwita alisema kutokana na kukosa udhamini katika ligi  ya kikapu ya mwaka huu, ni dalili tosha kwa mchezo huo kushindwa kuthaminiwa nchini, ikiwa ni tofauti na nchi nyingine maarufu kupitia kikapu.
“Inatusikitisha sana kwa kukosa nguvu ya kuendesha mashindano haya,kama unavyojuwa tuanjiendesha kupitia mfuko wetu wa Shirikisho hapa hatuna mdhamini ,kwa kifupi tuanjiendesha wenyewe tu, hii inaonyesha kiasi gani mchezo huu  ulivyokosa thamani hapa nchini,”alisema.
Alisema wanaitaka serikali kuwapa nguvu na kuipa kipaumbele mchezo wa mpira wa kikapu kama wanavyosaidia michezo mingine hapa nchini.
Mabingwa wa  nne wa michuano hiyo wataungana na mabingwa wa nne wa Zanzibar ambao wataenda kucheza kwenye kombe la Muungano ili kupata mabingwa wawili watakao wataenda kushiriki  mashindano ya Afrika mashariki,kaskazini na kusini(ZONE 5).

No comments:

Post a Comment