EBENEZA MARCH 9 2014

EBENEZA MARCH 9 2014

Wednesday, February 26, 2014

WITO KWA WAMILIKI WA MAENEO Y ABIASHARA: WAJASIRIAMALI WATAKIWA KUPEWA KIPAUMBELE

DSC_0935
Mwenyekiti wa Tancraft, Elihaika Mrema akizungumza na waandishi wa habari umuhimu wa jumuiya kubwa za wafanyabiashara na pamoja na serikali kuwaunga mkono wajasirimali wanawake nchini, Kushoto ni Esther Kasenga Msaidizi wa Katibu, Kulia Mweka hazina wa Chama cha Tancraft, Bi.Louise Judicate na Wapili kulia ni Katibu wa Tancraft, Bi. Vicky Shayo.
WAMILIKI Wote wa maeneo ya biashara nchini wameombwa kutoa nafasi ya maeneo ya biashara kwa wajasirimali wanawake ili kumkomboa mwanamke kutoka katika dimbwi la umaskini na utegemezi.
Akizungumza na waandishi wa habari pamoja na wajasirimali wanawake jijini Dar es Salaam leo mchana, Mwenyekiti wa Tanzania Handcraft Association (Tancraft), Elihaika Mrema amesema kuwa wanawake wafanyabiashara wadogo wana matatizo na changamoto kadhaa mojawapo ni maeneo ya kuuzia bidhaa zao.
“hata kama mjasirimali mwanamke ukimpa mtaji wa biashara na mafunzo changamoto kubwa ni kupata eneo la kuweza kuuza hiyo bidhaa yake aliyotengeneza kwa mikono yake mwenyewe,” amesema Mrema
DSC_0939
Pichani juu na chini ni Baadhi ya Wajasiriamali Wanawake wakifuatilia hotuba ya mwenyekiti wa TANCRAFT Bi. Elihaika Mrema alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari katika jengo la Biashara la DAR FREE MARKET lililopo barabara ya Ali Hassan Mwinyi karibu na Ubalozi wa Kenya nchini.

Mwenyekiti, Mrema amesema kuwa chama cha Tancraft kilianzishwa mwaka 2006 chini ya usimamizi wa Board of External Trade (BET) na Small industrial Development Organization (SIDO) na kina wanachama zaidi ya 300 kutoka mikoa yote Tanzania.
Amesema kuwa Tancraft ni chama cha wajasirimali wanaotengeneza bidhaa kwa kutumia mali ghafi za kutoka nchini kama vile nguo za batik, vikapu, minyaa, vitu vya ufinyanzi,vinyago, shanga, bidhaa za ngozi, chakula na usindikaji wa aiana zote zikiwemo asali.
DSC_0967
Hii ni moja ya zawadi ya kikombe kwa Chama cha Wajasiriamali Wanawake Tanzania (TANCFRAFT) walichowahi kupata kwa kuonyesha bidhaa zenye ubora wa kimataifa.
“malengo makuu ya chama yalikuwa ni pamoja na kuwatafutia wanachama wake soko la pamoja kwa ajili ya kuuzia bidhaa zao,” alilisisitiza Mrema Amesema kwamba chama cha wanawake wa wajasirimali kimepata sehemu ya Dar es Salaam Free Market ambapo wajasirimali wakinamama watapata fursa ya kufanya biashara zao bila kulipa ushuru kama walivyokuwa katika maeneo ya Chang’ombe mikono.

No comments:

Post a Comment