EBENEZA MARCH 9 2014

EBENEZA MARCH 9 2014

Friday, February 7, 2014

UWT: SHULE ZA KATA NI CHANZO UBAKAJI MKOANI MTWARA




Na: Kassim Ngumbi
Imebainika Kuwepo Kwa Shule Nyingi Za Kata Zisizokuwa Na Bweni Ni Sababu Za Ongezeko La Watoto Wengi Wa Kike Kubakwa Katika Maeno Mbalimbali Vijijini Kutokana Na Kutembea Umbali Mrefu Wakati Wa Kulekea Na Kurejea Toka Shuleni. Haya Yamelezw Na Mwenyekiti Wa Umoja Wa Wanawake Uwt Wilaya Ya Mtwara Katika Halmashauri Ya Mtwara Vijijini Ambaye Pia Ni Diwani Wa Viti Maalum Kata Ya Mahurunga Mh: Maimuna Lipulika Wakati Alipotembele Kata 28 Za Jimbo La Mtwara Vijijini Linaloongozwa Na Mh: Hawa Abdulahmani Ghasia Waziri Wa Nchi Ofisi Ya Waziri Mkuu Tawala Za Mikoa Na Serikali Za Mitaa (Tamisemi) Iliyochukua Siku Saba Akizungumza Na Mabaraza Ya Kata Ya Umoja Wa Wanawake Uwt Katika Ngazi Ya Wilaya, Ziara Yam H Lipulika Iliyobebwa Na Ajenda Tatu Ambazo Zot Zilikuwa Zinalenga Maendeleo Kwa Wanawake Ambazo Ni Kilimo,Ujasiriamali Na Elimu Huku Ajenda Ya Afya Ikiwa Ni Ajenda Ambayo Ni Nyongeza Aliwaeleza Wanawake Kuwa Elim Ni Muhimu Na Katika Utafiti Uliofanywa Imebainika Kuwa Mkoa Wa Mtwara Unaongoza Kwa Mimba Za Utotoni Kwa Wanafunzi Hasa Mtwwara Vijijini Na Hili Limekuwa Likijadiliwa Hata Kupitia Vikao Vya Baraza La Madiwani

La Halmashauri Na Wanawake Kwa Maana Ya Wazazi Na Walezi Wa Kike Wamekuwa Ndiyo Sababu Ya Kutokea Kwa Mimba Hizo Kani Mara Nyimgi Wamekuwa Wakiwafichia Siri Watoto Wao Wa Kike Bila Wazazi Wa Kiume Kufaham Lolote Na Inaptokea Akafaham Basi Wao Huwalinda Watoto Wao Hali Ambayo Inamanya Mtoto Ajiamini Kufanya Lolote Baya Kwa Elim Yake Kwa Wakati Wowoe Kama Vile Kujihusisha Na Mapenzi Bila Woga Na Mwisho Wa Siku Anajikuta Akipata Ujauzito. Lakini Pia Akaeleza Tatizo Linguine Ambalo Linaisumbua Mtwara Kuwa Ni Kutokuwepo Kwa Shule Zenye Kumwezesha Mwanafunzi Hasa Wa Kike Kulala Shuleni Kwani Shule Nyingi Zilizopo Mkoani Mtwara Ni Shule Za Kata Ambazo Hazina Mabweni Kwa Ajili Ya Wanafunzi Hali Hii Inasababisha Wanafunzi Kutembea Umbali Mrefu Kuelekea Shuleni Kwa Kutembea Kwa Mguu Au Wachache Kati Yao Kutumia Baisikeli Katika Ziara Hizo Za Shuleni Kila Siku Hali Ambayo Kwa Mtoto Wa Kike Ni Hatari Kwanza Inamtesa Kiafya Na Mazingira Lakini Pia Ni Sababisho La Wanafunzi Hao Kuingia Majaribuni Kutokana Na Watu Wasio Wema Kuwavizia Na Kutumia Fursa Ya Umbali Ukizingatia Eneo Kubwa Ni Vichaka Kuwashawishi Wanafunzi Kwa Kuwatongoza Na Kuwarubuni Kwa Vitu Mbalimbali Ikiwamo Fedha Na Zawadi Za Nguo, Na Inakua Ngumu Kwa Mtoto Kuepuka Mtego Huo Kwakua Mtongozaji Hupata Mda Mwingi Wa Kumshawishi Kwa Siku Tofautitoauti Na Mwisho Wa Siku Anafanikiwa Katika Kile Alichokusudia, Lakini Pia Hii Inawapa Mwanya Kundi Linguine La Watu Hao Wenye Nia Mbaya Kuwavizia Wanafunzi Wakike Njiani Na Kuwabaka Kutokana Na Matamanio Yao Hali Ambayo Ni Fedheha Kubwa Kwa Wanawake Na Mara Nyingi Inamharibu Mtoto Kisaikolojia Hata Kupelekea Kuchukua Maamuzi Magum Ya Kujiua Au Kuacha Shule Kutokana Na Aibu Na Kama Akiendelea Na Masomo Ni Lazima Ashuke Kiwango Kwani Mara Nyingine Wanafunzi Wenzake Humcheka Na Kumfanya Akose Raha.Katika Hili Amewaasa Wazazi Wakike Kuhakikisha Wanaandaa Mazingira Ya Ujenzi Wa Mabweni Katika Shule Zao Za Kata Kwa Kujitolea Na Baadae Serikali Itawasaidia Katika Hatua Zifuatazo Na Si Kuisubiri Serikali Pekeee Kufanya Kila Jambo Wakati Mwingine Maswala Mhim Kama Haya Ya Elim Wananchi Wanatakiwa Kushiriki Hasa Kwa Maslahi Ya Mtoto Wa Kike Wa Mkoa Wa Mtwara Na Tanzania Kwa Ujumla. Kwa Upande Wao Wakinamama Wa Kata Mbalimbali Ambazo Mh: Lipulika Ametembelea Wamekiri Kuwepo Kwa Hali Hizo Zote Na Kushauri Wazazi Wengine Ambao Wana Tabia Ya Kushiriki Na Watoto Wao Katika Kuficha Siri Ambazo Ni Athari Kwa Elim Ya Mtoto Na Afya Yake Kwa Ujumla Kuacha Mara Moja Na Kuanza Kupigania Haki Ya Mtoto Wa Kike Kwa Maendeleo Ya Taifa Wakati Mwingine Mambo Haya Huwa Yanapelekea Kutokea Kwa Ongezeko La Maambukizi Ya Virusi Vya Ukimwi Kwa Watoto Wakiwa Na Umri Mdogo Kabisa Na Kuwakatisha Tama Ya Kufikia Malingo Yao Waliyojiwekea Kupitia Elim Kwa Uzembe Wa Wazazi Wachache Wasio Na Malezi Mazuri Kwa Watoto Wao. Mwasho Lipulika Ameelekeza Viongozi Wa Mabaraza Ya Kata Ya Uwt Kuzungumza Na Matawi Yaliyoko Kwenye Kata Zao Juu Ya Masuala Haya Ili Kubadili Muonekano Wa Elim Ya Sasa Mkoani Mtwara Toka Mimba Nyingi Na Matukio Ya Ubakaji Pamoja Na Kufeli Kwa Wanafunzi Na Kwenda Hatua Nyingine Ambayo Ni Ya Maendeleo.
SIKILIZA HAPA HOTUBA YA MWENYEKITI UWT MTWARA

No comments:

Post a Comment