EBENEZA MARCH 9 2014

EBENEZA MARCH 9 2014

Saturday, February 1, 2014

NANI KAONDOKA?NANI KAINGIA? DIRISHA DOGO LA USAJILI ULAYA



Na mshamu ngojwike
PAZIA la usajili wa dirisha dogo Ulaya limefungwa usiku wa Jana na ifuatayo ni taarifa ya usajili wa klabu zote za England, wachezaji waliotemwa na kusajiliwa.
ARSENAL: Imesajili mchezaji mmoja tu, Kim Kallstrom kwa mkopo kutoka Spartak Moscow, wakati walioondoka ni Chuba Akpom (Brentford, mkopo), Anthony Jeffrey (Wycombe, mkopo), Benik Afobe (Sheffield Wednesday, mkopo), Nico Yennaris (Brentford) Emmanuel Frimpong (Barnsley), Daniel Boateng (Hibernian, mkopo), Park Chu-Young (Watford, mkopo).






kocha wa manchester united David Moyes akimsainisha Juan Mata
ASTON VILLA: Waliosajiliwa ni Grant Holt (Wigan, mkopo) na Ryan Bertrand (Chelsea, mkopo), wakati walioondoka ni Stephen Ireland (Stoke), Michael Drennen (Carlisle, mkopo) na Jordan Graham (Bradford, mkopo).

CARDIFF: Waliosajiliwa ni Magnus Wolff Eikrem (Heerenveen, Pauni Milioni 2), Mats Moller Daehli (Molde), Jo Inge Berget (Molde), Kenwyne Jones (Stoke, kubadilishana), Fabio da Silva (Manchester United), Wilfried Zaha (Manchester United, mkopo). Walioondoka ni Rudy Gestede (Blackburn), Filip Kiss (Ross County, mkopo), Nicky Maynard (Wigan, mkopo), John Brayford (Sheffield Utd, mkopo), Peter Odemwingie (Stoke, kubadilishana), Simon Moore (Bristol City, mkopo), Craig Conway (Blackburn Rovers, mkopo) na Andreas Cornelius (FC Copenhagen).

CHELSEA: Waliosajiliwa ni Bertrand Traore (Association Jeunes Espoirs De Bobo-Dioulasso), Nemanja Matic (Benfica, Pauni Milioni 21), Mohamed Salah (Basel Pauni Milioni 11) na Kurt Zouma (Saint Etienne, Pauni Milioni 12.5), wakati walioondoka ni Bertrand Traore (Vitesse Arnhem, mkopo), Kevin de Bruyne (Wolfsburg, Pauni Milioni 17), Ryan Bertrand (Aston Villa, mkopo) Josh McEachran (Wigan, mkopo), Juan Mata (Manchester United, Pauni Milioni 37.1) Michael Essien (AC Milan), Sam Walker (Colchester, mkopo), Nathaniel Chalobah (MIddlesbrough, mkopo), Kenneth Omeruo (Middlesbrough, mkopo), Patrick Bamford (Derby, mkopo) na Gael Kakuta (Lazio, mkopo).


                   Bertrand Traore karibu chelsea mwana

CRYSTAL PALACE: Waliosajiliwa ni Jason Puncheon (Southampton), Scott Dann (Blackburn), Wayne Hennessey (Wolves, Pauni Milioni 3), Tom Ince (Blackpool, mkopo) na Joe Ledley (Celtic), wakati walioondoka ni Jason Banton (Plymouth, huru), Jimmy Kebe (Leeds, mkopo), Kwesi Appiah (Notts County, mkopo), Matt Parsons (Plymouth), Jack Hunt (Barnsley, mkopo) na Jose Campana (Nuremburg, mkopo).

EVERTON: Waliosajiliwa ni Aiden McGeady (Spartak Moscow), Lacina Traore (Monaco, mkopo) na Jindrich Stanek (Sparta Prague) wakati walioondoka ni Nikica Jelavic (Hull), Matthew Kennedy (Tranmere, mkopo), Shane Duffy (Yeovil, mkopo), Hallam Hope (Northampton, mkopo), Chris Long (MK Dons, mkopo), Matthew Pennington (Tranmere, mkopo) na Johnny Heitinga (Fulham, huru).

FULHAM: Waliosajiliwa ni Clint Dempsey (Seattle Sounders, mkopo), William Kvist (mkopo, Stuttgart), Lewis Holtby (Tottenham, mkopo), Konstantinos Mitroglou (Olympiacos, Pauni Milioni 12.4) na Johnny Heitinga (Everton, huru), wakati walioondoka ni Bryan Ruiz (PSV, mkopo), Stephen Arthurworrey (Tranmere, mkopo), Marcus Bettinelli (Accrington, mkopo), Jack Grimmer (Port Vale, mkopo), Aaron Hughes (QPR, undisclosed), Dimitar Berbatov (Monaco, mkopo).

HULL: Waliosajiliwa ni Nikica Jelavic (Everton), Elliott Kebbie (Atletico Madrid, mkopo), Shane Long (West Brom, Pauni Milioni 6), wakati walioondoka ni Tom Cairney (Blackburn, Pauni 500,000), Conor Townsend (Carlisle, mkopo), Eldin Jakupovic (Leyton Orient, mkopo), Cameron Stewart (Leeds, mkopo), Nick Proschwitz (Barnsley, mkopo), Gedo (Al Ahly) na Aaron Mclean (Bradford).

LIVERPOOL: Hakuna aliyesajiliwa, wakati walioondoka ni Adam Morgan (Yeovil, huru), Tiago Ilori (Granada, mkopo), Craig Roddan (Accrington Stanley, mkopo), Ryan McLaughlin (Barnsley, mkopo) na Michael Ngoo (Walsall, mkopo).

MANCHESTER CITY: Hakuna aliyesajiliwa wakati walioondoka ni John Guidetti (Stoke, mkopo), Albert Rusnak (Birmingham mkopo), Emyr Huws (Birmingham, mkopo) na Abdisalam Ibrahim (ametemwa).

MANCHESTER UNITED; Aliyesajiliwa ni Juan Mata pekee kutoka Chelsea kwa Pauni Milioni 37.1), wakati walioondoka ni Jack Barmby (Hartlepool, mkopo), Anderson (Fiorentina), Fabio da Silva (Manchester United), Wilfried Zaha (Cardiff, mkopo), Fabio da Silva (Cardiff), Tom Lawrence (Yeovil Town, mkopo), Tyler Blackett (Birmingham City, mkopo), Sam Byrne (Carlisle United, mkopo), Charni Ekangamene (Carlisle United, mkopo), Tom Thorpe (Birmingham City, mkopo), Federico Macheda (Birmingham City, mkopo), Will Keane (QPR, mkopo) na San Johnstone (Doncaster Rovers, mkopo).

NEWCASTLE; Aliyesajiliwa ni Luuk de Jong (Borussia Monchengladbach, mkopo) pekee, wakati walioondoka ni Yohan Cabaye (Paris-Saint Germain, Pauni Milioni 23), Jonas Gutierrez (Norwich, mkopo), Curtis Good (Dundee United, mkopo).

NORWICH; Imemsajili Jonas Gutierrez pekee kwa mkopo kutoka Newcastle, wakati walioondoka ni Daniel Ayala (Middlesbrough, Pauni 350,000) na Jamar Loza (Leyton Orient, mkopo).

SOUTHAMPTON; Hakuna aliyesajiliwa wakati walioondoka ni Lee Barnard (Southend, mkopo), Danny Fox (Nottingham Forest, mkopo), Billy Sharp (Doncaster, mkopo), Dani Osvaldo (Juventus, mkopo), Jason Puncheon (Crystal Palace).

STOKE; Waliosajiliwa ni John Guidetti (Man City, mkopo), Stephen Ireland (Aston Villa), Juan Agudelo (New England Revolution), wakati walioondoka ni Brek Shea (Barnsley, mkopo), Jamie Ness (Leyton Orient, mkopo) na Juan Agudelo (FC Utrecht, mkopo).

SUNDERLAND; Waliosajiliwa ni Marcos Alonso (Fiorentina, mkopo), Santiago Vergini (Estudiantes, mkopo), Oscar Ustari (Almeria), Ignacio Scocco (Internacional, Pauni Milioni 3), Liam Bridcutt (Brighton, Pauni Milioni 2.5), wakati walioondoka ni Mikael Mandron (Fleetwood, mkopo), Ji Dong-won (Augsburg), Billy Knot (Port Vale, mkopo), Cabral (Genoa, mkopo), Modibo Diakite (Fiorentina, mkopo), David Moberg Karlsson (Kilmarnock, mkopo), David Vaughan (Nottingham Forest, mkopo) na Duncan Watmore (Hibernian, mkopo).

        Jembe jipya la arsenal kim kallstrom

SWANSEA; Waliosajiliwa ni David Ngog (Bolton), Raheem Hanley (Blackburn), Jay Fulton (Falkirk) na Marvin Emnes (Middlesbrough, mkopo), wakati walioondoka ni Alan Tate (Aberdeen, mkopo), Daniel Alfei (Portsmouth, mkopo), Rory Donnelly (Coventry City, mkopo)

TOTTENHAM; Hakuna aliyesajiliwa wakati walioondoka ni Jermain Defoe (Toronto, Pauni Milioni 6), Simon Dawkins (Derby), Shaquile Coulthirst (Leyton Orient, mkopo), Jon Obika (Brighton, mkopo), Ryan Fredericks (Millwall, mkopo), Adam Smith (Bournemouth), Lewis Holtby (Fulham, mkopo).

WEST BROMWICH ALBION; Aliyesajiliwa ni Thievy Bifouma pekee kutoka Espanyol kwa mkopo,wakati walioondoka Lee Camp (Bournemouth), Shane Long (Hull, Pauni Milioni 6), George Thorne (Derby, mkopo).

WEST HAM: Waliosajiliwa ni Roger Johnson (Wolves, mkopo), Antonio Nocerino (Milan), Marco Borrielo (Roma, mkopo) Abdul Razak (Anzhi Makhachkala), Pablo Armero (Napoli, mkopo), wakati waliosajiliwa ni Blair Turgott (Rotherham, mkopo), Jordan Spence (MK Dons, mkopo), Paul McCallum (Hearts, mkopo) na Modibo Maiga (QPR, mkopo).


 

 

MIYEYUSHO SIWEZI PANDA ULINGONI BILA MKATABA


NA MSHAMU NGOJWIKE
BONDIA Francis Miyeyusho amegoma kupanda ulingoni kwenye pambano lake dhidi ya Viktor Chernous wa Ukraine hadi atakapo atakapopewa mkataba na promota wa pambano hilo.
               bondia francis miyeyusho       

Pambano hilo lilipangwa kufanyika Februari 8 mwaka huu kwenye Ukumbi wa PTA Sabasaba jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na SWACOTZ FORUM,Miyeyusho alisema amekatazwa na kocha wake kuanza maandalizi ya pambano hilo wakati bado hawajakubaliana chochote na promota Jay msangi.

“Hadi sasa sijauoana mkataba wa pambano hilo,sasa nitaanzaje kufanya mazoezi wakati hatujafanya mazungumzo ya makubaliano na promota,”alisema

  
     miyeyusho kazini
Pambano hilo limepangwa kufanyika siku moja na lile la bondia Francis Cheka dhidi ya Brudov wa Urusi 8 kwenye uzani wa light heavy kg 81 la  kuwania ubingwa wa WBF International.

No comments:

Post a Comment