HALI YA SOKO KUU MTWARA IKO HIVI |
NA:VERONICA VICTOR
Mvua zinazoendelea
kunyesha Mkoani Mtwara zimesababisha baadhi ya wakazi wa Manispaa ya Mtwara
Mikindani, kupoteza makazi yao na kusababisha usumbufu mkubwa unaotokana na
maji kujaa katika nyumba zao.
Aidha mvua hizo
zimefanya wananchi hao kupoteza vyakula na mali, huku wafanyabiashara nao wakiwa katika wakati
mgumu baada ya biashara zao na maeneo wanayofanyia biashara hizo kuingiliwa na
maji.
Mwandishi wa habari wa
pride fm alijionea hayo leo asubuhi wakati alipotembelea maeneo yaliyoathirika
ya magomeni bomba la bure, chuno na soko kuu katika Manispaa ya Mtwara.
SOKO LA MBOGAMBOGA MTWARA |
Wakizungumza na
mwandishi huyo kwa nyakati tofauti wakazi wa magomeni bomba la bure wamesema
kuwa tatizo la maji kujaa limesababishwa na ujenzi wa barabara, lilipowekwa
kalavati lenye tundu dogo linaloshindwa kupitisha maji kwa urahisi, na sababisha maji hayo kujaa na kuingia
katika nyumba za watu.
MAENEO YA MAKAZI YA WATU |
Aidha kwa upande wa
mwenyekiti wa soko kuu la Manispaa ya mtwara Bw Ramandhani licheta, amekiri kuwa hali ya soko hairidhishi hususani eneo linalotumika kwa
biashara za mboga na matunda, kwa kuwa halina uwezo wa kutoa maji yatokanayo na
mvua.
HALI NDIYO HII |
No comments:
Post a Comment