EBENEZA MARCH 9 2014

EBENEZA MARCH 9 2014

Wednesday, February 19, 2014

Mgombea wa Chadema Kalenga amwekea pingamizi wa CCM

Mgombea ubunge Jimbo la Kalenga kwa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Grace Tendega.
Mgombea ubunge Jimbo la Kalenga kwa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Grace Tendega amemuwekea pingamizi mgombea mwenzake kutoka Chama cha Mapinduzi (CCM),  Godfrey Mgimwa kwa kile anachodai kuwa siyo raia wa Tanzania.

Tendega alichukua fomu ya kumwekea pingamizi mgombea huyo wa CCM juzi na jana majira ya mchana alirudisha  fomu hiyo kwa msimamizi wa uchaguzi  huo, Pudensiana Kisaka.

 Akizungumza na NIPASHE jana, Mratibu wa Chadema Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Frank Mwaisumbe alisema mgombea wa chama hicho amemuwekea pingamizi mgombea wa CCM baada ya kubaini kwamba siyo raia wa Tanzania.

Alidai sababu nyingine ni Mgimwa kupeleka wadhamini ambao siyo wakazi wa Jimbo la Kalenga na siyo wapiga kura wa jimbo hilo.

"Kielelezo kingine ni tarehe ya uteuzi wa mgombea wa CCM kuwa batili ambapo ilitajwa kuwa tarehe 16 badala ya 18" alisema Mwaisumbe.

Alipoulizwa na NIPASHE kwa njia ya simu juu ya suala hilo, Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Kalenga, Pudensiana Kisaka alithibitisha kuwa mgombea mgombea huyo wa Chadema amemwekea pingamizi mgombea wa CCM, lakini akasema hawezi kutolea maelezo yoyote kwa kuwa ndiyo kwanza taratibu zinafanyika.
 
CHANZO: NIPASHE

No comments:

Post a Comment