EBENEZA MARCH 9 2014

EBENEZA MARCH 9 2014

Wednesday, February 19, 2014

KINYEREZI SASA UMEME WA KUMWAGA MEGAWATI 150 KUANZA KUZALISHWA

Eliakim Maswi
Wizara ya Nishati na Madini kupitia Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), imepokea mashine mbili za kufua umeme zenye gharama ya Dola za Marekani milioni 52.

Mashine hizo zitakuwa na uwezo wa kufua umeme wa megawati 75, kufuatia utekelezaji wa ahadi ya serikali kufikisha megawati 150.

Meneja Miradi wa Tanesco, Simon Jilima, alisema baada kuteremshwa mashine hizo, zitahifadhiwa Kinyerezi na zoezi la kuzifunga litaanza Februari 28, mwaka huu.
Alisema mradi huo utagharimu Dola za Marekani milioni 183 na unatarajiwa kukamilika Oktoba, mwaka huu.

 Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Eliakim Maswi, alisema shehena hiyo ni ya awamu ya kwanza ikiwa ni sehemu ya kuondoa mitambo chakavu ya kufua umeme.

“Nategemea shehena nyingine mwezi ujao yenye vifaa kama hivi kutoka nchini Marekani ili kufikisha idadi ya megawati 150,” alisema.
 
CHANZO: NIPASHE

No comments:

Post a Comment