EBENEZA MARCH 9 2014

EBENEZA MARCH 9 2014

Wednesday, January 29, 2014

Tuhuma za Zitto Kabwe ( CHADEMA ) kutoka kimapenzi na mbunge Catherine Magige ( CCM ) ni za uongo na zimepikwa kwa lengo la kumchafua.



KUNDI la watu ambao inadaiwa kwamba wamekula yamini ya kumchafua Mbunge wa Kigoma Kaskazini (Chadema), Zitto Kabwe kwa namna yoyote ile, wamemuonjesha machungu Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Mkoa wa Arusha, Catherine Magige.
Zitto, baada ya msululu wa tuhuma ambazo nyingi zilibainika kupikwa makusudi ili kuichafua taswira yake mbele ya jamii, sasa hivi anahusishwa kutoka kimapenzi na Magige, ikidaiwa kuwa walisafiri pamoja kwenda Dubai kwa ajili ya kufanya mambo yasiyofaa.
Hata hivyo, uchunguzi uliofanywa na gazeti LA Uwazi umebaini kuwa tuhuma hiyo ya Zitto na Magige ni nyingine kati ya zile zilizopikwa, kwani ukweli wake ni wa kufikirika.


Imebainika kuwa safari ya Dubai ambayo inasemwa kuwa Zitto na Magige walisafiri, inapotoshwa kwa sababu ukweli ni kwamba wabunge hao walisafiri pamoja na timu nzima ya Kamati ya Hesabu za Serikali Bungeni (PAC) kwa shughuli za kikazi na hakukuwa na suala la mapenzi kati yao.
Mbunge wa Ludewa (CCM), Deo Filikunjombe, aliye makamu mwenyekiti wa PAC, akiizungumzia skendo hiyo ya Zitto na Magige alisema: “Nimeona ujumbe ambao unasambazwa kuhusu Zitto na Catherine (Magige), ni uongo mkubwa, hakuna kitu kama hicho.
“Nimeona wanazungumzia zaidi tiketi, ni kweli tulisafiri kamati nzima kwenda Dubai. Wajumbe wote wa PAC tulikwenda Dubai baadaye Uingereza. Zitto ndiye hakwenda Uingereza, yeye aliishia Dubai na kurudi nchini.
“Katika hili namsikitikia zaidi Magige kwa sababu anaingizwa kwenye vita ambayo haijui, siyo mzoefu wa kashfa hizi za kuzushiwa, Zitto angalau naweza kusema amezoea. Nitasimama kokote kumtetea Catherine na hata Zitto. Hili limeandaliwa makusudi kumchafua Zitto na hii ni vita ndani ya Chadema wao kwa wao.”
Mjumbe wa PAC, Esther Matiko, ambaye ni Mbunge wa Viti Maalum (Chadema) Mkoa wa Mara, alisema: “Hilo suala ni la uongo kabisa, walioanzisha hiyo tuhuma pengine wanataka kumchafua Catherine. Tulifikia hoteli moja na chumba changu na kile cha Catherine, vilikuwa karibukaribu, hakuna kitu kama hicho kinachosemwa.
“ Catherine alisafiri na mwanaye wa kike anayesoma kidato cha kwanza, na alikuwa akilala naye chumba kimoja, sasa hayo mambo yangewezekanaje? Hizi ni siasa tu. Kwanza Catherine hii siyo safari yake ya kwanza, kila tunaposafiri kwenda nje, huwa analala chumba kimoja na dada Lucy (Owenya, Mbunge wa Viti Maalum Chadema).
“Kitendo cha kupendelea kulala chumba kimoja na dada Lucy maana yake hapendi hayo mambo, tena ni kuonesha anaogopa manenomaneno kama haya. Safari zote huwa analala na dada Lucy, kasoro hiyo tu ndiyo alilala na mwanaye wa kike. Zaidi ya hayo, namsemea Zitto, yeye ni mwenyekiti wetu, amekuwa akitaka tuwe na maadili ndiyo maana hajawahi kuwa na uhusiano na mjumbe yeyote.”
Zitto hakupatikana kuzungumzia tuhuma hiyo lakini Catherine alipopatikana alisema kuwa hana maneno kwa sababu anajua kinachosemwa ni uongo, akaongeza: “Wanatishia wana video, waiweke wazi kama ni kweli. Hizi siasa za kuchafuana kwa vitu vya uongo hazifai hata kidogo, haziisaidii nchi.”

Source: Gazeti la uwazi/ gpl
.......
Gharama hizo ni maalum kwa ajili ya wakazi waishio jirani na bomba hilo linaloanzia Mtwara hadi Dar es Salaam kupitia mikoa ya Lindi na Pwani.
Akizungumza na mamia ya wakazi wa Mangaka waliofika kushuhudia uzinduzi huo, Waziri Mkuu alisema uzinduzi wa mradi huo wa umeme ni utekelezaji wa azma ya Serikali ya kuhakikisha kila wilaya inapata umeme.
“Mpango wa kupeleka umeme nchi nzima ni wa miaka mitatu na katika sekta ya Nishati chini ya Mpango wa Matokeo Makubwa ya Haraka (BRN), tumeazimia kwenda kwa awamu ili tuwafikie wananchi wengi zaidi kutoka asilimia 24 ya sasa hadi kufikia asilimia 30 ya watumiaji wa umeme,” alisema Waziri Mkuu.
Akitoa taarifa juu ya mradi huo wa umeme wilayani Nanyumbu, Meneja Mwandamizi wa TANESCO, Kanda ya Dar es Salaam na Pwani inayojumuisha mikoa ya Lindi na Mtwara, Eng. Mahende Mugaya alisema mradi huo umegharimu sh. bilioni 5.6/- na unatarajiwa kukamilika Aprili, mwaka huu.
Alisema kuzinduliwa kwa mradi huo kunafanya wilaya zote za mkoa wa Mtwara ziwe zimepata umeme wa kuanzia na kwamba kazi itaendelea kupitia Wakala wa Umeme Vijijini (REA) ili kuongeza idadi ya watumiaji wa umeme kwenye mkoa huo.
“Chini ya mfuko wa REA tumetenga sh. bilioni 7.6 ili zitumike kusambaza umeme katika wilaya zote za mkoa wa Mtwara ambao sasa hivi watumiaji wa umeme wamefikia 15,675 sawa na asilimia nne ya wakazi wote wa mkoa huu.”


Alisema katika mwaka 2012-2013 walipata wateja 2,609 tofauti na idadi ya zamani ya wateja 1,300 ambayo ilikuwa imezoeleka. Alisema hivi sasa wamepokea maombi kutoka kwa wateja 2,588 ambao tayari wamekwishalipia gharama za kuunganishiwa umeme.
Chini ya mradi wa umeme kupitia REA, jumla ya vijiji 54 katika wilaya za Tandahimba, Masasi na Newala vitanufaika na mradi huo ulioanza kutekelezwa Desemba 2013 na unatarajiwa kukamilika ifikapo Desemba 2015.

SERIKALI imeamua kupunguza kwa kiasi kikubwa bei ya kuunganisha umeme majumbani na kufikia sh. 27,000/ kwa wanavijiji wanaoishi kwenye maeneo ambayo bomba la gesi linapita.
Hatua hiyo imetangazwa jana (Jumapili, Januari 26, 2014), na Waziri wa Nishati na Madini, Prof. Sospeter Muhongo wakati akizungumza na wanakijiji wa Mangaka wilayani Nanyumbu, mkoani Mtwara kabla ya kumkaribisha Waziri Mkuu, Mizengo Pinda azindue mradi wa umeme kwenye wilaya hiyo.
“Jana Waziri Mkuu aliagiza tutafute namna ya kuwasaidia wananchi wanaoishi jirani na njia ya bomba la gesi. Nami nilikaa na wasaidizi wangu jana usiku na kufanya hesabu na tukaamua tuweke kiwango hicho kwa ajili ya wakazi hao,” alisema.
Alisema katika mikoa mikoa mingine gharama za kuunganisha umeme ni sh. 177,000/- lakini kwa mikoa ya Lindi na Mtwara gharama hizo zilishushwa na kufikia sh.99,000/-. “Lakini sasa hawa wenzetu tumewapa upendeleo zaidi na tumewapunguzia gharama hizo hadi sh. 27,000/-,” alisema huku akishangiliwa.



1 comment: