EBENEZA MARCH 9 2014

EBENEZA MARCH 9 2014

Sunday, January 19, 2014

TBS kuwasaka waingizaji wa nguo za ndani


Mitumba nguo za ndaniSHIRIKA la Viwango Tanzania (TBS) litafanya operesheni ya kuwasaka wale wote wanaoingiza nguo za ndani za mitumba nchini.
Akizungumza na Tanzania Daima Jumapili jana, Ofisa Mahusiano wa TBS, Roida Andusamile, alisema kuwa hivi sasa wameanza kuwakamata wafanyabiashara wadodo wadogo katika masoko mbalimbali ya jijini Dar es Salaam ili kubaini zinapotoka nguo hizo.
Alisema kuwa nguo hizo zimepigwa marufuku kutokana na kuwa na athari za kiafya hivyo hazihitajiki kuingizwa sokoni.
Andusamile alizitaja nguo ambazo zimepigwa marufuku ni pamoja na soksi, nguo za ndani kwa wanawake na wanaume, pamoja sidiria.
“Kufanya biashara hii ni kosa kubwa kwa kuwa zinahatarisha maisha ya Watanzania ambao hawana hatia, pia sheria iko wazi ambayo ilipitishwa mwaka 2003 ikipiga marufuku uingizaji wa nguo hizi,” alisema.
Alisema kuwa katika msako wa wafanyabiashara ndogo ndogo walikamata nguo hizo katika manispaa zote za jijini na kulazimika kuziteketeza.
Alisema kuwa kuwa endapo wakikamata mfanyabiashara mdogo asipotoa ushirikiano anakozipata nguo hizo atalazimika kulipa faini ya sh milioni 50 hadi 100.
SOURCE: TANZANIA DAIMA

No comments:

Post a Comment