EBENEZA MARCH 9 2014

EBENEZA MARCH 9 2014

Sunday, January 26, 2014

NUSU FAINALI YA CHAN 2014 YATIMIA


CHAN2014_LOGORobo Fainali za CHAN 2014, Mashindano ya Mataifa ya Afrika kwa Wachezaji wanaocheza ndani ya Nchi zao tu, zimekamilika kwa Libya na Ghana kufuzu kuingia Nusu Fainali na kuungana na Zimbabwe na Nigeria waliofuzu Jumamosi.
Kwenye Mechi ya Awali, Dakika 90 za Robo Fainali kati ya Gabon na Libya ilimalizika kwa suluhu ya 1-1 baada Libya kutangulia kufunga katika Dakika ya 50 kupitia Abdelsalam Omar na Daniel Cousin kuisawazishia Gabon Dakika ya 74 kwa Penati baada ya Fetori kumvuta Lionel Yackouya na Mechi kwenda Dakika za Nyongeza 30 bila mabadiliko.
Kwenye Mikwaju ya Penati, baada Dakika 120, Libya walitoka Washindi kwa Penati 4-2 baada kufunga Penati zao zote 4 na Gabon kukosa 2 na kutinga Nusu Fainali ambapo Jumatano watacheza na Zimbabwe.
Katika Mechi iliyofuatia, Penati ya Dakika ya 68 ya Kwabina Adusei imewapeleka Ghana Nusu Fainali baada ya kuifunga Congo DR Bao 1-0.
Penati hiyo ilitolewa baada ya Kimwika wa Congo DR kuunawa Mpira kwenye Boksi.
Kwenye Nusu Fainali Jumatano ijayo, Ghana watawavaa Wapinzani wao wa Jadi Nigeria.
VIKOSI:
Ghana: Adams; Adusei (Azumah 70’), Ainooson, Sulley, Tijani; Akuffo (Owusu 82’), Mpong (Attorbah 53’), Opoku; Mohammed, Anobaah, Bansey
Congo DR: Kidiaba; Litombe, Kasusula, Muselenge, Kimwaki; Nsimbi, Ndombe (Mukanisa 85’), Basisila (Emomo 72’), Mundele; Mabidi, Mavuanga (Nzinga 63’)
ROBO FAINALI
Jumamosi Januari 25
[Cape Town Stadium]
Morocco 3 Nigeria 4 [3-3 baada Dakika 90]
Mali 1 Zimbabwe 2
Jumapili Januari 26
[SAA za Bongo]
Gabon 1 Libya 1 [Pia 1-1 Baada Dakika 120, Libya yashinda Penati 4-2]
Ghana 1 Congo DR 0
NUSU FAINALI
Jumatano Januari 29
[SAA za Bongo]
1800 Zimbabwe v Libya [Free State Stadium]
2130 Ghana v Nigeria [Free State Stadium]
Jumamosi Februari 1
[SAA za Bongo]
1800 Mshindi wa Tatu [Cape Town Stadium]
2100 Fainali [Cape Town Stadium]

No comments:

Post a Comment