![]() |
RAIS wa SMZ DK,Shein kushoto akiwa na katibu mkuu wa CCM Abdullahman Kinana Visiwani Zanziba |
0Zanzibar. Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana amesema ameamua kuweka kambi Zanzibar, lengo likiwa ni kuimarisha chama hicho na kuhakikisha CCM inarejesha majimbo yake yaliyopotea tangu kuanzishwa kwa mfumo wa vyama vingi mwaka 1995.
Kinana aliweka msimamo huo kwenye mkutano wa
hadhara wa uzinduzi wa miaka 37 ya kuzaliwa CCM, uliofanyika uwanja wa
Soka Kiembesamaki mjini hapa juzi.
Alisema kambi hiyo itaanza kabla ya Aprili mwaka
huu, kwa kufanya ziara kuanzia ngazi ya wadi, jimbo, wilaya hadi mikoa
kukagua hali ya kisiasa na kuweka mikakati mipya ya chama hicho kisiwani
Zanzibar.
“Nitaanza ziara maalumu kabla ya sherehe za
Muungano, mengi nitayazungumza wakati huo ukifika, lengo kubwa ni
kuangalia uhai wa chama chetu na kuweka mikakati ya kisiasa kabla ya
mwaka,” alisema Kinana.
Alisema kazi kubwa ya CCM ni kutekekeza sera na
ilani yake ya uchaguzi tofauti na vyama vya upinzani, ambavyo ni mahiri
na hodari wa kusema bila ya kuonyesha vitendo.
Katibu Mkuu huyo aliviponda vya upinzani nchini na
kwamba, CCM imewaachia kazi ya kusema, yenyewe imekijikita kuwatumia
wananchi na kutekeleza majukumu yake ya kisera, mipango na mwongozo.
Kuhusu Mapinduzi ya Zanzibar ya mwaka 1964, Kinana
alisema watu waliobeza Mapinduzi hayo hivi sasa wamefedheheka kwa
kushuhudia yakitimiza miaka 50 huku taifa likiwana hali ya amani, umoja
na mshikamano.
“Waliodhani Mapinduzi yatashindwa wameshindwa
wao.Tumejiimarisha kwa ulinzi na usalama, tumejenga umoja, upendo na
maelewano, kubwa tukijivunia hatua za maendeleo yaliofikiwa, ” alisema
Kinana.
Tangu kuanzishwa kwa mfumo wa vyama vingi mwaka
1992 na kufuatiwa na uchaguzi mkuu wa kwanza mwaka 1995, CCM ilipata
pigo kubwa kwa kupoteza viti vyote majimbo Pemba na wakati ikitafakari
hayo, CCM ikaendelea tena kupoteza viti vyake vya Magogoni, Mtoni na
Nungwi kisiwani Unguja mwaka 2010.
Viongozi waliohudhuria mkutano huo wa uzinduzi wa
miaka 37 ya kuzaliwa kwa CCM, ni Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar, Dk
Ali Mohamed Shein, Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar, Balozi Seif Ali Idd,
Spika wa Baraza la Wawakili (BLW), Pandu Ameir Kificho na Naibu Katibu
Mkuu wa CCM Zanzibar, Vuai Ali Vuai.
Wakati maadhimisho hayo yakifanyika mjini hapa,
uchaguzi mdogo wa uwakilishi Jimbo la Kiembesamaki unatarajiwa kufanyika
Jumapili hii.
Uchaguzi huo unafanyika kufuatia CCM kumfukuza
uanchama, aliyekuwa mwakilishi wa jimbo hilo, Mansoor Yusuf Himid kwa
tuhuma za kwenda kinyume na mlengo wa chama hicho. Alikuwa akipigania
kurejeshwa kwa Serikali ya Zanzibar yenye mamlaka. Baba yake ni miongoni
mwa waasisi wa Mapinduzi.
No comments:
Post a Comment