Hayo yalikuwa maneno ya kocha, Alex Ferguson,
aliyoyatamka pale Old Trafford katika hotuba yake ya kuwaaga wachezaji
na klabu ya Manchester United mwishoni mwa msimu uliopita. Ilikuwa ni
baada ya kuitumikia klabu hiyo kwa miaka 27.
Wote – wachezaji, viongozi na washabiki walionekana kumuunga mkono kwa dhati kocha mpya, David Moyes.
Kweli msimu ukaanza, Manchester United ikaifunga
Swansea, lakini mashabiki wakaonekana kuwa naye hata katika shida pale
Manchester City ilipowakung’uta mabao 4-1 na pia walipopigwa mfululizo
na Everton na Newcastle.
Hadi Ijumaa ya wiki iliyopita hali ya hewa ilikuwa
imechafuka Old Trafford kwani Mashetani Wekundu walikuwa wamekubali
vipigo vitatu mfululizo.
Katika maanguko yao, Mashetani Wekundu wamekuwa
wakisema kwamba hakuna tatizo kwani watarudi katika kiwango na kusonga
mbele na ushindi.
Hata hivyo, baadhi ya wadau wameanza kupata hisia
na mawazo tofauti juu ya klabu, baada ya kujiuliza tatizo lipo wapi
wakati kikosi ni kilekile cha msimu uliopita alichokiacha Ferguson?
Tena kuna nyongeza ya Wilfred Zaha aliyekuwa ameachwa kwa mkopo Crystal Palace baada ya kusajiliwa na kocha huyo aliyepita.
Sasa kuna wanaodai tatizo lipo kwa kocha Moyes na
kwamba kama wanataka kurudi juu katika nafasi walizozizoea, lazima
wachukue uamuzi mgumu kwa kumwondosha kwa madai kwamba hakuwa chaguo
sahihi.
Je, Bodi ya Wakurugenzi ya Manchester United
itakaa na kukiri kwamba walifanya makosa kukubali ushauri wa Ferguson
kwa kumteua Mskochi mwenzake, kisha wamwite Moyes, wamshukuru kwa
‘jitihada’ zake na kuachana naye?
Baadhi ya takwimu zinawashitua mashabiki wa
Manchester United na wadau wengine wa soka, kwa sababu katika miaka 27
ya ukocha wa Ferguson ni mara moja tu timu hiyo ilitolewa katika raundi
ya tatu ya Kombe la FA, lakini Moyes katika miezi yake sita ameshatolewa
tayari katika raundi hiyo.
Swansea ilitia doa historia ya Manchester United
maana ushindi wake wa Januari 5 ndio wa kwanza kuupata Old Trafford
tangu timu hiyo ilipoanzishwa.
SOURCE: MWANASPORT
SOURCE: MWANASPORT
No comments:
Post a Comment