EBENEZA MARCH 9 2014

EBENEZA MARCH 9 2014

Tuesday, January 28, 2014

KESI YA MAMILIONI YA IPTR KUANZA KUNGURUMA FEBRUARI 24

Dar es Salaam. Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Februari 24, 2014 itaanza kusikiliza ushahidi wa kesi ya wizi wa mafuta yenye thamani ya Sh 970.6 milioni ya kulainisha mitambo ya kampuni ya Independent Power Tanzania Limited (IPTL), inayowakabili watu wanane.

Washtakiwa wanaokabiliwa na kesi ni Simon Theobard maarufu kama Kadudu, Ally Maulid, Mussa Rajabu, Kessy Charles, Alan Mtweve, Peter Ngongolo, Frank Mpepo na Idd Yusuphu.
Wakili wa Serikali, Aida Kisumo alimwambia Hakimu Mkazi, Emilius Mchauru anayeisikiliza kesi hiyo kuwa jana ilitakiwa kuanza kusikilizwa, lakini shahidi wa upande wa mashtaka hajui lugha ya Kiswahili.
Hivyo waliandika barua Bakita kuomba msaada wa kupata mkalimani Desemba 16, 2013 lakini hadi sasa hawajapata taarifa yoyote.
Katika kesi hiyo, washtakiwa hao kwa pamoja wanakabiliwa na mashtaka mawili likiwamo la kula njama ya kutenda kosa la wizi.
Inadaiwa kuwa kati ya Desemba Mosi na mbili, 2011 wakiwa eneo la Tegeta Wilaya ya Kinondoni waliiba lita 62,800 za mafuta ya kulainishia mitambo ya IPTL zenye thamani ya Sh 970.6milioni.

No comments:

Post a Comment