Nicolaus Miseny-M/kiti mpira wa mikono TZ |
NAmsham ngojwike
Chama cha Mpira wa
mikono Tanzania (TAHA) kimeanza mchakato wa kurejesha mchezo huo kwa wananchi baada
ya kutopewa kipaumbele kama michezo mingine kwa takribani miaka 20.
Mwenyekiti wa TAHA
Nicolause Mihayo aliliambia BINGWA jana kuwa urejeshwaji wa mchezo huo utaanza
katika shule za msingi na Sekondari hapa nchini.
“Mchezo huu umekuwa
haupewi kipaumbele hapa nchini jambo linalosababisha kuanza kupotea sasa chama
kimeamu kuurudisha ili uwe kama zamani ambapo hadi itakapofika mwakani tuwe
tumepiga hatua kubwa katika mpango huu,”alisema.
Alisema kuwa
Tanzania imekuwa nchi ya kwanza kucheza mchezo wa mpira wa mikono Afrika
Mashariki na Kati miaka ya 60, watalamu wengi kutoka nchini wamekuwa wakisafiri
kwenda kuzifundisha nchi zingine huku hapa nchi ukizidi kupotea.
Mihayo alisema kuwa
hadi sasa ni mkoa wa Mbeya pekee ndio
uliobakia ambapo tayari wameshakuwa tayari kuanza kupokea mafunzo hayo katika
shule zao.
Amewaomba watua
wanaoufahamu mchezo huo kujitolea kutoa elimu ili waweze kuyafikia malengo yao
na kuufanay mchezo huo kuwa miongoni kwa michezo inayopewa kipaumbele.
No comments:
Post a Comment