Pamoja na nchi ya Rwanda kuwa katika shinikizo la kimataifa, kuhusu
tuhuma za kuwafadhili waasi wa kundi la M23 waliokuwa wakipambana na serikali
ya DRC, nchi hiyo imeendeleza ukimya wa hali ya juu tangu kushindwa kwa kundi
hilo.
Mapema siku ya
Jumanne kundi hilo lilitangaza kuhitimisha miezi 18 ya uasi wake, baada ya
kushindwa vibaya na kuangukia mikononi mwa majeshi ya Jamhuri ya Kidemokrasia
ya Kongo (FARDC) wakisaidiwa na kikosi maalumu cha Umoja wa Mataifa.
Kwa sasa waasi hao wako chini ya shinikizo la
kusaini rasmi makubaliano ya amani kesho Jumatatu nchini Uganda, nchi ambayo
wapiganaji wengi wa kundi hilo, wamekimbilia huku idadi kubwa ya wapiganaji
waliojeruhiwa wamekimbilia nchini Rwanda.Wataalam wa Umoja wa Mataifa wamekuwa wakiishutumu kwa kuwaunga mkono kwa kiasi fulani waasi hao, licha ya mataifa hayo kukanusha vikali madai hayo.
No comments:
Post a Comment