EBENEZA MARCH 9 2014
SWACO
royal
tt
NIMO
mvuto
Wednesday, July 17, 2013
KILWA YACHAFUKA MAONI YA KATIBA
Wajumbe kutoka kata 21 za wilaya kilwa mkoani Lindi waliounda baraza la katiba la wilaya nusura wazipige kufuatia mvutano kuhusu nafsi ya waziri mkuu kwenye serikali ya shirikisho katika katiba ijayo.
Tukio hilo lilitokea baada ya mwenyekiti wa kundi la sita la tume prof
Palamagamba Kabudi lilipokuwa wilayani kilwa ambapo walichangia
kutokana na makundi yalioanishwa Katika makundi hayo yalipewa hoja kujadili ambapo kundi na moja lilipewa hoja ya maadili lingine mihimili ya dola pamoja na , haki za binadamu na suala la uwepo wa Muungano,
Akichangia maoni yake kwenye kundi lilokuwa likijadili suala la
Maadili, bw Shaibu mohamedi Nginji alieleza kuwa uwepo wa serikali ya shirikisho hakuna umuhimu wa kuwa na waziri mkuu kwa kuwa majukumu yake yatafanywa na makamu wa rais
“hakuna haja ya kuwa na waziri mkuu kwani kufanya hivyo ni sawa na kurudi kwenye muungano wa serikali mbili, jambo ambalo aliwezi kukubalika kwa kuwa hakuna sababu ya kuogopa muundo wa serikali tatu na ndio utakuwa ukombozi wetu watu wa bara”.
Hoja hiyo ilipingwa na wajumbe wengine wa kundi liloongozwa na Haji
Ibrahimu na kusababisha kurushiana maneno na wajumbe wengine kususia mjadala na kuwaachia wachache wakiendelea kujadili .
Mvutano huo ulipata ufumbuzi baada ya mwenyekiti wa kundi la sita la
tume Prof Paramaganda Kabudi kuwataka wajumbe hao kutambua kuwa kila mjumbe aliekuwepo kwenye kikao hicho ana haki ya kuchangia mawazo yake ili mradi havunji sheria za Nchi na kufanya hivyo ndio maana ya kuunda katiba ya Wananchi baada ya kutoa maoni yao.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment