MBUNGE wa
Kinondoni (CCM), Idd Azzan, amesema yupo tayari kujiuzulu ubunge, ikiwa
itabainika anajihusisha biashara ya dawa za kulevya. Kauli hiyo imekuja
siku chache baada ya kutajwa katika moja ya barua iliyosambazwa katika
mitandao ya kijamii, baada ya mtu anayedaiwa kukamatwa China na
kuwatuhumu watu kadhaa akiwamo Idd Azzan.
Akizungumza na
MTANZANIA jana kuhusu sakata hilo, alisema hatua ya kuhusishwa na
biashara haramu ya dawa za kulevya, ni kutotenda haki mbele ya jamii
hasa wapiga kura wake na Taifa kwa ujumla.
Alisema mtu aliyendika barua ya tuhuma dhidi yake, ni wazi amedhamiria kumshushia heshima na huenda akawa ana...
JACK WOLPER AMJIBU MBAYA WAKE ALIYETANGAZA KUWA YEYE NI KAHABA
Msanii nyota wa filamu bongo, Jacqueline Wolper amewataka wasanii
wa bongo movie kuacha tabia ya kupigana majungu ya kinafiki
ambayo huchangia kujenga bifu za kijinga....
Akiongea na mpekuzi wetu, wolper alidai kuwa kuna mipaka ya
watu kuishi lakini kuna baadhi ya wasanii wanaamini kwamba
majungu ndo mshahara wao kiasi kwamba wasipomsengenya mtu basi
hawawezi ...
UKOO WATISHIWA KUTEKETEZWA KWA USHIRIKINA HUKO TABORA
Watu watatu wa ukoo mmoja wameuawa kwa kukatwa mapanga
kutokana na imani za kishirikina katika Wilaya ya Nzega Tabora, huku
ujumbe mkali wa kuuawa kwa watu wengine ukiachwa katika Kijiji cha
Nsanga.
Tukio hilo lilitokea katika kijiji hicho kilichopo
Kata ya Ikindwa Nzega, Julai 25 mwaka huu, ambapo Mkuu wa Wilaya ya
Nzega Bituni Msangi alisema sababu ya mauaji hayo ni kukithiri kwa imani
za kishirikina kwa baadhi ya wananchi wa kijiji hicho.
Aliwataja waliouawa kuwa ni Catherin Shija (65),
Fransnc Kaliki (69) pamoja na Maria Kulwa (52) wote wakiwa ni wa ukoo
mmoja wakiishi katika kijiji hicho.
Akizungumza na wananchi wa kijiji hicho alisema
watu wanaofanya mauaji hayo...
No comments:
Post a Comment