EBENEZA MARCH 9 2014

EBENEZA MARCH 9 2014
Showing posts with label TUPE MUONO WAKO KATIKA HILI. Show all posts
Showing posts with label TUPE MUONO WAKO KATIKA HILI. Show all posts

Friday, January 17, 2014

KIONGOZI WA JUMUIA YA KIROHO YA BOHRA DUNIANI AFARIKI DUNIA AKIWA NA MIAKA 102

IKULU, DAR ES SALAAM
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete ametuma salamu za rambirambi kwa Jumuia ya Dawoodi Bohra katika Tanzania kufuatia kifo cha Kiongozi wa Kiroho wa Jumuia hiyo duniani, Dkt. Seydna Mohammed Burhanuddin (Pichani), ambaye amefariki dunia asubuhi ya Ijumaa, Januari 17, 2014.

Dkt. Seydna Mohammed Burhanuddin, Kiongozi wa Jumuia ya Dawoodi Bohra kwa miaka 39 iliyopita,  amefariki dunia nyumbani kwake katika kasri ya Saifee Mahal, eneo la Mahabar, kusini mwa jiji la Mumbai, India, kwa ugonjwa wa moyo akiwa na umri wa miaka 102.

Katika salamu zake kwa Mwenyekiti wa Jumuia ya Dawoodi Bohra katika Tanzania, Sheikh Tayabali Sheikh Hamzabhai Patanwalla, Rais Kikwete amesema: “Nimepokea kwa huzuni na masikitiko taarifa za kifo cha Dkt. Seydna Mohammed Burhanuddin, Kiongozi wa Kiroho wa Jumuia ya Dawoodi Bohra duniani kwa miaka mingi ambacho nimejulishwa kimetokea subuhi ya leo nyumbani kwake mjini Mumbai, India.”