NA MSHAMU
NGOJWIKE
TIMU ya Ndanda Fc, jana ilianza vyema michezo yake
ya kirafiki baada ya kuifunga JKT Ruvu kwa mabao 4-1,kwenye Uwanja wa Chuo
Kikuu cha Ardhi jijini Dar es Salaam.
Ndanda Fc
imeweka kambi ya siku 40 katika Chuo Kikuu Cha Ardhi jijini,Dar es Salaam,ikiajiandaa
na Ligi Kuu Tanzania Bara mwaka huu.
![]() |
| DENIS KITAMBI KOCHA NDANDA FC |
Mchezo
huo wa kujipima ubavu, ulikuwa wa kuonyeshana ufundi huku kila kocha akitumia
vikosi viwili ili kutambua ubora wa timu yake.
Lakini
Ndanda Fc walionekana kuukamia mchezo
huo, baada ya kuonyesha kandanda safi na pasi za kuonana,kupitia kwa wachezaji
wao waliowasajili msimu huu.
Mabao ya
Ndanda Fc yalifungwa na Jacob Masawe,Nassoro Kapama,Rajabu Isihaka na
Mshambuliaji Mnigeria Lukman Abegunrin,huku la JKT Ruvu lilifungwa na Saidi
Dihile.
Akizungumza
na SWACOTZ FORUM,Kocha Msaidizi wa Ndanda Fc, alisema kuwa amefurahishwa na uwezo
walioonyesha wachezaji kwenye mchezo wa leo,na atatumia fursa ya kurekebisha makosa aliyoyaona katika
mchezo huo.
“Wachezaji
wamecheza Vizuri hata kama kuna mapungufu madogo madogo ambayo nitakaa na
kuyatafutia ufumbuzi kabla ya kucheza mechi nyingine ya kirafiki,”alisema.
Alisema kuanzia
wiki ijayo watatumia muda mwingi wa kucheza mechi za kirafiki na timu ambazo
zinashiriki Ligi kuu Tanzania Bara,ili kukitambua vizuri kikosi chake.

No comments:
Post a Comment