Baada ya mizengwe kibao, hatimaye mshambuliaji nyota wa Borussia Dortimund, Robert Lewandowski ametua katika kikosi cha Bayern Munich.
Lewandowski, amesaini mkataba wa miaka mitano na mabingwa hao wa Ujerumani, klabu aliyokuwa na ndoto ya kuichezea lakini kukawa na mizengwe iliyotawala.
Mkali huyo amefunga mabao 74 na kusababisha 31 katika mechi zake 131 za Bundesliga akiwa na Dortmund aliyojiunga nayo mwaka 2010 akitokea klabu ya Lech Poznan ya nchini kwake Poland.
No comments:
Post a Comment