MJUMBE wa Bunge Maalumu la Katiba, Assumpta Mshama, ameishambulia
Tume ya Mabadiliko ya Katiba na kusema kuwa licha ya usomi wa wajumbe
waliopo, lakini wameandaa kitu ambacho kinataka kuwagawa Watanzania.
Mshama alitoa kauli hiyo bungeni jana alipokuwa akichangia hoja za kamati kwenye rasimu ya pili ya katiba.
Alisema kuwepo na serikali tatu ni kutoa kauli ambayo ni ya uzandiki,
ugombanishi, fitina na chuki na haimpendezi Mungu hata kidogo.
Mbarouk Salum Ally, alihoji hofu ya CCM kuhusu uwepo na serikali tatu inatokana na nini.
Sambamba na hilo alishangazwa na tabia ya baadhi ya Wazanzibar kugeuza kauli wanapofika Dodoma.
“Ndugu zetu wa Zanzibar ambao ni wanaCCM wakifika huku sijui
mnawafanya nini, wakitoka Zanzibar wanakuwa wazima, wakija huku
wanakuwa kama mboga za viazi.
“Mheshimiwa mwenyekiti wanawadanganya, wakitoka hapa wanalalamika Muungano unawanyonya na hauwatendei haki,” alisema.
Mhandisi Pamela Masai, alisema kauli ya serikali ya kusema Tanzania ina amani haina ukweli.
“Serikali inategemea watu watoke na mapanga barabarani ndiyo wajue amani hakuna?” alihoji mjumbe huyo.
No comments:
Post a Comment