Mkurugenzi wa Benki ya CRDB, Dk Charles Kimei.
Akizindua huduma hiyo katika kilele cha maadhimisho ya miaka 43 ya KCMC, Mkurugenzi wa Benki ya CRDB, Dk Charles Kimei alisema kwa kutambua umuhimu wa upatikanaji wa huduma sahihi za afya na kutokomeza utapeli pamoja na rushwa, benki yake imeamua kuja na huduma mpya ya matibabu kwa kutumia kadi maalum.
Alisema kadi hiyo itasaidia kupunguza matatizo mengi ya wananchi yakiwemo kutapeliwa, usumbufu wa kupata huduma ya afya pamoja na vifo visivyotarajiwa.
“Kumekuwa na matukio mengi ya vifo visivyotarajiwa vinavyotokana na wagonjwa kukosa fedha za kugharamia matibabu hasa inapotokea dharura huku ndugu jamaa na marafiki wakiwa mbali, leo tunazindua huduma mpya ya kulipia kwa njia ya kadi, tunaamini kwa huduma hii wagonjwa wengi wataweza kutibiwa kwa haraka zaidi,” alisema Kimei.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa fedha wa KCMC, Hilda Mungure, alisema uzinduzi wa huduma hiyo katika kipindi hiki ambacho hospitali inakabiliwa na changamoto ya wingi wa wateja, ni mkombozi mkubwa na itasaida kupunguza foleni za kulipia gharama za matibabu na kupunguzakero za wagonjwa.
CHANZO:
NIPASHE
No comments:
Post a Comment