![]() |
MAKAMU M/KITI BODI YA KOROSHO TANZANIA MH: MUDHIHIRI MUDHIHIRI AKIZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI (Picha na maktaba) |
NA: VERONICA VICTOR…..Mtwara
Akitoa taarifa hiyo kwa vyombo vya habari Makamu
Mwenyekiti wa Bodi ya Korosho Tanzania Mudhihiri Mudhihiri amesema kuwa katika
msimu huu uzalishaji umekuwa wa tani 124,966.098 kutoka tani 127,947.49 za
msimu uliopita.
Amesema kuwa pia bei ya korosho hizo ilikuwa sh 1402
kwa kilo hadi sh 1723 na zaidi ya asilimia 70 ya korosho zote zilizouzwa kwa
bei ya 1500 za kitanzania kwa waliozingatia mfumo wa stakabadhi ghalani.
Aidha amesema
ubora wa korosho ghafi daraja la kwanza msimu huu umeongezeka hadi kufikia
asilimia 99 ukilinganisha na asilimia 90 ya msimu uliopita, na ongezeko hilo
umetokana na matumizi sahihi ya pembejeo, uelewa wa wakulima juu ya mfumo wa
stakabadhi mazao ghalani, pamoja na kuepuka wakulima kulipwa kwa awamu.
Ameeleza kuwa Bodi kwa kushirikiana na taasisi ya
utafiti wa kilimo naliendele pamoja na mfuko wa wakfu wa kuendeleza zao la
korosho mkoani humo, wataendesha mafunzo ya ugani kwa wakulima ili kuwawezesha
kutumia pembejeo za kilimo kwa ufanisi unaotakiwa kwa ajili ya kuongeza
uzalishaji.
No comments:
Post a Comment