“Homa ya Ini ni ugonjwa hatari sana, maana ukimpata mtu kinachofuata ni kifo. Naweza kusema ni ugonjwa hatari zaidi kuliko hata Ukimwi, lakini tofauti yake na Ukimwi ni moja; huu una kinga. “Ni lazima tuungane kama taifa, huu ugonjwa ni hatari sana, sisi Global Publishers tumeanza, kinachofaa ni wewe na yule kujitokeza ili tuishinde hii vita pamoja. Leo tunaizindua rasmi,” alisema Shigongo na kuongeza: “Ndugu zetu wengi sana wanapoteza maisha kila siku kutokana na ugonjwa huu wa Homa ya Ini, lakini kwa sababu chanjo ipo, lazima tuchukue hatua.
Sisi Global Publishers tumeamua kuchukua jukumu la kuhakikisha Hepatitis B unatokomezwa.” Kampeni hii inaendeshwa na Global Publishers kwa kushirikiana na Hospitali ya Amana, Megra Clinic, Sanofi Pasteur, Damu Salama na SD Africa.
No comments:
Post a Comment