EBENEZA MARCH 9 2014

EBENEZA MARCH 9 2014

Tuesday, March 11, 2014

FIGO YATAJWA KUWA NI UGONJWA HATARI SANA NCHINI TANZANIA HUKU GHARAMA ZA MATIBABU YAKE ZIKIWA JUU SANA MILL:8


Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii,Dk. Seif Rashid.
Idadi ya wagonjwa wanaogua ugonjwa sugu wa figo, imeendelea kuongezeka nchini kutokana na gharama kubwa ya matibabu pamoja na kukosekana kwa huduma ya kupandikiza figo.

Gharama za matibabu inayotolewa hapa nchini kwa wagonjwa wa figo ni Shilingi milioni nne kwa mwezi kwa kila mgonjwa.

Takwimu za Chama cha Figo Duniani zinaonyesha kuwa mwanaume mmoja kati ya watano na mwanamke mmoja kati ya wanne walio katika umri wa miaka 65 hadi 74, huugua ugonjwa huo.

Hayo yalisemwa na Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Seif Rashid, wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana kuhusu maadhimisho ya Siku ya Afya ya Figo Duniani.

Aidha, Dk. Seif alisema kuwa asilimia 10 ya watu wote wameathirika pamoja na vifo vya asilimia moja vinavyotokea duniani hutokana na ugonjwa sugu wa figo.

Waziri Seif alisema idadi ya wagonjwa wa ugonjwa huo, imeendelea kukua kutokana na watu kutofanya mazoezi, kuwa na uzito, unene uliokithiri ambao unasababiswa na ulaji usiofaa hususan matumizi ya chumvi pamoja na sukari nyingi ikiwamo mafuta.

Alizitaja sababu nyingine kuwa ni unywaji pombe kupita kiasi, uvutaji wa bidhaa zitokanazo na tumbaku, sigara, shinikizo la damu na msongo wa mawazo.

Alisema kuwa katika maadhimisho yatakayofanyika mkoani Dodoma, Machi 13, mwaka huu, Wizara itatoa elimu na huduma ya kupima afya ya figo, kutoa ushauri nasaha ikiwamo kutoa tiba na rufaa kwa wananchi.

Maadhimisho ya mwaka huu kauli mbiu yake ni ‘Figo huzeeka kadiri mtu anavyozeeka. Jali afya ya figo zako.’
 

CHANZO: NIPASHE


No comments:

Post a Comment