EBENEZA MARCH 9 2014

EBENEZA MARCH 9 2014

Monday, March 17, 2014

CHADEMA YAMWAGA SIRI ZA KALENGA YASEMA USHINDI WA CCM SI WA HALALI HATA KIDOGO

Wakati Chama Cha Mapinduzi (CCM) kikisheherekea ushindi wake wa ubunge katika Uchaguzi Mdogo Jimbo la Kalenga uliofanyika juzi, Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimedai kuwa chama tawala kimeshinda kwa hila kutokana na kuwatumia watu kutoka sehemu mbalimbali.
Wakati Chama Cha Mapinduzi (CCM) kikisheherekea ushindi wake wa ubunge katika Uchaguzi Mdogo Jimbo la Kalenga uliofanyika juzi, Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimedai kuwa chama tawala kimeshinda kwa hila kutokana na kuwatumia watu kutoka sehemu mbalimbali pamoja na makamanda wa chama hicho Green Guard kumpigia kura mgombea wao.

Msimamizi wa uchaguzi huo, Pudencian Kisaka, jana, alimtangaza mgombea wa CCM, Godfrey Mgimwa kuwa mshindi kwa kupata kura 22,972 (asilimia 79), Grace Tendegu wa Chadema kura 5,853 (asilimia 20) na Richard Mimja wa  Chausta kura 150 (asilimia 0.52).

Baada ya matokeo hayo kutangazwa, Mkurugenzi wa Operesheni na Oganaizesheni wa Chadema, Benson Kigaila, alisema matokeo kilichopata chama chake siyo halali kwa madai  CCM walitumia watu kutoka sehemu mbalimbali kumpigia kura Mgimwa.

 “Chadema hatukubaliani na matokeo haya kwa sababu sisi tulitaka wananchi wa Kalenga wapige kura kwa amani, lakini amani hiyo imetoweka kutokana na CCM kutumia vikundi vyao vya ulinzi Green Guard na watu wengine kuwapigia kura,” alisema Kigaila.

Alidai kuwa CCM kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi mkoani Iringa waliwafukuza watu kutoka vituo vya upigaji kura na wengine kupigwa.

Alidai kuwa baadhi ya wafuasi wa Chadema walitekwa na CCM kwa kushirikiana na Polisi na kwamba baadhi walipigwa na kujeruhiwa akiwamo Mbunge wa Viti Maalumu, Rose Kamili.

Alidai kuwa CCM walifanya vitendo hivyo siku ya uchaguzi na kwamba waliteka gari la Chadema likiwa na viongozi wake wawili Walter Wanuo, mkazi wa Mianzini na Edward Julius, mkazi wa Namanga mkoani Arusha na kuwapeleka kusikojulikana.

  “Siku ya uchaguzi askari polisi walikuwa wakikagua magari ya Chadema wakidhani kuwa tumebeba silaha, kumbe hatujabeba silaha zozote, lakini askari hao hawakukagua gari lolote la CCM wakati wao ndio waliokuwa wamebeba kila aina ya silaha,” alidai.

Kigaila alidai kuwa gari lililotekwa ni Prado namba T. 808 AMX likiwa na viongozi hao na kupelekwa katika ofisi ya CCM mkoa wa Iringa na baadaye liliondolewa na kwamba hawajui lilipo.

“Sisi Chadema hatuondoki Iringa hadi Jeshi la Polisi lituambie wapi wamepeleka gari letu na viongozi pamoja na vijana waliotekwa ndipo tuondoke,” alisema Kigaila na kuongeza kuwa Kamati Kuu itatoa tamko baadaye kuhusiana na uchaguzi huo.

CHANZO: NIPASHE

No comments:

Post a Comment