EBENEZA MARCH 9 2014

EBENEZA MARCH 9 2014

Thursday, March 6, 2014

BARUA YA DAVID MOYES KWA MASHABIKI WA MAN U


MOYES_MASIKITIKODAVID MOYES amewaandikia Mashabiki wa Manchester United kuwashukuru kwa sapoti yao kubwa huku akikiri kuwa Msimu huu umekwenda ovyo kupita walivyofikiria.
Meneja huyo, ambae ndie Msimu wake wa kwanza Old Trafford baada kurithi nafasi ya Sir Alex Ferguson ambae alistaafu Mwezi Mei baada ya Miaka 26, amekuwa na mwanzo mbovu na Man United, ambao ndio Mabingwa Watetezi wa Ligi Kuu England, wapo Nafasi ya 7 kwenye Ligi na wameshuhudia vipigo vitano Old Trafford tangu Moyes atwae hatamu.
Katika Barua hiyo, Moyes ameandika: “Ingawa nilijua kazi hii ni changamoto kubwa wakati naichukua, Msimu huu mgumu sio kitu nilichofikiria kama nyinyi Mashabiki ambavyo sasa mnafikiria, na sasa Wachezaji wangu, Wafanyakazi na mimi tutahaha kulipa fidia kwa hilo.MOYES-A_WORD_FROM_THE_BOSS
“Nyinyi mmezoea kuona mafanikio Manchester United na sapoti mliyowapa Wachezaji na mimi Msimu huu wote hauna mfano. Nje ya Nyumbani Mashabiki wanaosafiri na Timu wamekuwa bora kuliko wote Nchi nzima na hapa Old Trafford hamyumbi na tunafarijika sana.”

“Kusapoti Timu yako ikiwa inashinda ni kitu rahisi lakini ni ngumu mno ikiwa mambo yanaenda kombo na uzalendo wenu mlioonyesha hauna kifani.”
Moyes aliendelea kwa kutamka uhakika wake kwamba: “Kila kitu tulichopitia kitatuimarisha zaidi, kuifanya Timu imara na Klabu bora baadae. Kwa Miaka mingi mmeona Vikosi imara vikishinda hapa, na, katika muda, nina hakika kabisa tutaona Vikosi imara vikishinda tena hapa.”
MAN UNITED-Mechi zijazo 4:
[Ligi Kuu England isipokuwa inapotajwa]
Machi 8 West Bromwich v Man United
Machi 16 Man United v Liverpool
Machi 19 Man United v Olympiacos [UEFA CHAMPIONZ LIGI]
Machi 22 West Ham v Man United

No comments:

Post a Comment