EBENEZA MARCH 9 2014

EBENEZA MARCH 9 2014

Thursday, February 20, 2014

Pakistan yawaua Taliban 15


Kiongozi wa Taliban nchini Pakistan Fazlullah
Maafisa wa usalama nchini Pakistan wanasema kuwa washukiwa 15 wanaotuhumiwa kuwa wapiganaji wameuwawa katika shambulizi la jeshi la wanahewa.
Ndege za kivita za Pakistan zilishambulia maeneo ya kaskazini magharibi mwa nchi hiyo maeneo yanayoshukiwa kuwa ngome na maficho yakundi la Taliban .
Mashambulizi hayo katika Jimbo la Waziristan yanatizamwa na wandani wa maswala ya Mashariki ya mbali kama njia ya jeshi la taifa kulipiza kisasi shambulizi lililosababisha vifo vya wanajeshi kadhaa mapema wiki hii.
Mapema juma hili muafaka wa amani uliokuwa ufanyike kati ya serikali na wapiganaji wa Taliban yalisambaratika baada ya kundi moja linalounga mkono Taliban, kusema kuwa limewauwa wanajeshi 23 waliokuwa wamewateka.
Ripoti kutoka mji wa Mir Ali zinasema kuwa wapiganaji wa kigeni ni miongoni mwa wale waliouawaa katika mashambulizi haya ya usiku Kucha.

No comments:

Post a Comment