WAJANJA kaeni chonjo! Mbeya City imetangaza vita kwa kuanzisha msako mkali wa wafanyabiashara wanaouza jezi na bidhaa zenye rangi na nembo zake.
Muda mfupi baada ya kuonekana ina mafanikio katika
Ligi Kuu Bara, jezi na skafu za Mbeya City zimekuwa zikiuzwa kwa wingi
katika miji mbalimbali nchini bila timu hiyo kunufaika.
Kutokana na hali hiyo, klabu hiyo inayomilikiwa na
Halmshauri ya Jiji la Mbeya, imeweka watu wake maalumu wanaozunguka
mitaani katika majiji mbalimbali kuwabaini watu wanaouza bidhaa zenye
nembo yao bila makubaliano maalumu.
Akizungumza na Mwanaspoti, Ofisa Habari wa Mbeya
City, Fred Jackson alisema wameweka mkakati huo baada ya kubaini kuwepo
kwa watu wachache wanaonufaika na jina la klabu hiyo huku wao wakiwa
hawanufaiki.
“Kuna watu wanauza jezi zenye nembo yetu ambayo ni
alama ya Halmashauri ya Jiji la Mbeya jambo ambalo ni hatari kwani
wanaonufaika ni wao na si sisi ambao tunaihudumia timu kwa kila hali.
“Kuanzia sasa mtu tutakayemkamata anauza bidhaa
hizo tutampeleka mahakamani ili akakumbane na sheria maana huo ni wizi
wa wazi,” alisema Fred kwa msisitizo.
Wafanyabiashara mbalimbali hapa nchini wamekuwa na
tabia ya kutengeneza jezi zenye nembo za klabu mbalimbali za ligi kuu
na kuziuza bila ya makubaliano yoyote na viongozi wa timu hizo.
SOURCE:MWANASPORT
SOURCE:MWANASPORT
No comments:
Post a Comment