Zitto,
baada ya msululu wa tuhuma ambazo nyingi zilibainika kupikwa makusudi ili
kuichafua taswira yake mbele ya jamii, sasa hivi anahusishwa kutoka kimapenzi
na Magige, ikidaiwa kuwa walisafiri pamoja kwenda Dubai kwa ajili ya kufanya
mambo yasiyofaa.
Hata
hivyo, uchunguzi uliofanywa na gazeti LA Uwazi umebaini kuwa tuhuma hiyo ya
Zitto na Magige ni nyingine kati ya zile zilizopikwa, kwani ukweli wake ni wa
kufikirika.
Imebainika
kuwa safari ya Dubai ambayo inasemwa kuwa Zitto na Magige walisafiri,
inapotoshwa kwa sababu ukweli ni kwamba wabunge hao walisafiri pamoja na timu
nzima ya Kamati ya Hesabu za Serikali Bungeni (PAC) kwa shughuli za kikazi na
hakukuwa na suala la mapenzi kati yao.
Mbunge
wa Ludewa (CCM), Deo Filikunjombe, aliye makamu mwenyekiti wa PAC,
akiizungumzia skendo hiyo ya Zitto na Magige alisema: “Nimeona ujumbe ambao
unasambazwa kuhusu Zitto na Catherine (Magige), ni uongo mkubwa, hakuna kitu
kama hicho.
“Nimeona
wanazungumzia zaidi tiketi, ni kweli tulisafiri kamati nzima kwenda Dubai.
Wajumbe wote wa PAC tulikwenda Dubai baadaye Uingereza. Zitto ndiye hakwenda
Uingereza, yeye aliishia Dubai na kurudi nchini.
“Katika
hili namsikitikia zaidi Magige kwa sababu anaingizwa kwenye vita ambayo haijui,
siyo mzoefu wa kashfa hizi za kuzushiwa, Zitto angalau naweza kusema amezoea.
Nitasimama kokote kumtetea Catherine na hata Zitto. Hili limeandaliwa makusudi
kumchafua Zitto na hii ni vita ndani ya Chadema wao kwa wao.”
Mjumbe
wa PAC, Esther Matiko, ambaye ni Mbunge wa Viti Maalum (Chadema) Mkoa wa Mara,
alisema: “Hilo suala ni la uongo kabisa, walioanzisha hiyo tuhuma pengine
wanataka kumchafua Catherine. Tulifikia hoteli moja na chumba changu na kile
cha Catherine, vilikuwa karibukaribu, hakuna kitu kama hicho kinachosemwa.
“
Catherine alisafiri na mwanaye wa kike anayesoma kidato cha kwanza, na alikuwa
akilala naye chumba kimoja, sasa hayo mambo yangewezekanaje? Hizi ni siasa tu.
Kwanza Catherine hii siyo safari yake ya kwanza, kila tunaposafiri kwenda nje,
huwa analala chumba kimoja na dada Lucy (Owenya, Mbunge wa Viti Maalum Chadema).
“Kitendo
cha kupendelea kulala chumba kimoja na dada Lucy maana yake hapendi hayo mambo,
tena ni kuonesha anaogopa manenomaneno kama haya. Safari zote huwa analala na
dada Lucy, kasoro hiyo tu ndiyo alilala na mwanaye wa kike. Zaidi ya hayo,
namsemea Zitto, yeye ni mwenyekiti wetu, amekuwa akitaka tuwe na maadili ndiyo
maana hajawahi kuwa na uhusiano na mjumbe yeyote.”
Zitto
hakupatikana kuzungumzia tuhuma hiyo lakini Catherine alipopatikana alisema
kuwa hana maneno kwa sababu anajua kinachosemwa ni uongo, akaongeza:
“Wanatishia wana video, waiweke wazi kama ni kweli. Hizi siasa za kuchafuana
kwa vitu vya uongo hazifai hata kidogo, haziisaidii nchi.”
Source: Gazeti la uwazi/ gpl
.......
Gharama
hizo ni maalum kwa ajili ya wakazi waishio jirani na bomba hilo linaloanzia
Mtwara hadi Dar es Salaam kupitia mikoa ya Lindi na Pwani.
Akizungumza
na mamia ya wakazi wa Mangaka waliofika kushuhudia uzinduzi huo, Waziri Mkuu
alisema uzinduzi wa mradi huo wa umeme ni utekelezaji wa azma ya Serikali ya
kuhakikisha kila wilaya inapata umeme.
“Mpango
wa kupeleka umeme nchi nzima ni wa miaka mitatu na katika sekta ya Nishati
chini ya Mpango wa Matokeo Makubwa ya Haraka (BRN), tumeazimia kwenda kwa awamu
ili tuwafikie wananchi wengi zaidi kutoka asilimia 24 ya sasa hadi kufikia
asilimia 30 ya watumiaji wa umeme,” alisema Waziri Mkuu.
Akitoa
taarifa juu ya mradi huo wa umeme wilayani Nanyumbu, Meneja Mwandamizi wa
TANESCO, Kanda ya Dar es Salaam na Pwani inayojumuisha mikoa ya Lindi na
Mtwara, Eng. Mahende Mugaya alisema mradi huo umegharimu sh. bilioni 5.6/- na
unatarajiwa kukamilika Aprili, mwaka huu.
Alisema
kuzinduliwa kwa mradi huo kunafanya wilaya zote za mkoa wa Mtwara ziwe zimepata
umeme wa kuanzia na kwamba kazi itaendelea kupitia Wakala wa Umeme Vijijini
(REA) ili kuongeza idadi ya watumiaji wa umeme kwenye mkoa huo.
“Chini
ya mfuko wa REA tumetenga sh. bilioni 7.6 ili zitumike kusambaza umeme katika
wilaya zote za mkoa wa Mtwara ambao sasa hivi watumiaji wa umeme wamefikia
15,675 sawa na asilimia nne ya wakazi wote wa mkoa huu.”
Alisema
katika mwaka 2012-2013 walipata wateja 2,609 tofauti na idadi ya zamani ya
wateja 1,300 ambayo ilikuwa imezoeleka. Alisema hivi sasa wamepokea maombi
kutoka kwa wateja 2,588 ambao tayari wamekwishalipia gharama za kuunganishiwa
umeme.
Chini
ya mradi wa umeme kupitia REA, jumla ya vijiji 54 katika wilaya za Tandahimba,
Masasi na Newala vitanufaika na mradi huo ulioanza kutekelezwa Desemba 2013 na
unatarajiwa kukamilika ifikapo Desemba 2015.
SERIKALI imeamua kupunguza kwa kiasi kikubwa bei ya kuunganisha umeme majumbani
na kufikia sh. 27,000/ kwa wanavijiji wanaoishi kwenye maeneo ambayo bomba la
gesi linapita.
Hatua
hiyo imetangazwa jana (Jumapili, Januari 26, 2014), na Waziri wa Nishati na
Madini, Prof. Sospeter Muhongo wakati akizungumza na wanakijiji wa Mangaka
wilayani Nanyumbu, mkoani Mtwara kabla ya kumkaribisha Waziri Mkuu, Mizengo
Pinda azindue mradi wa umeme kwenye wilaya hiyo.
“Jana
Waziri Mkuu aliagiza tutafute namna ya kuwasaidia wananchi wanaoishi jirani na
njia ya bomba la gesi. Nami nilikaa na wasaidizi wangu jana usiku na kufanya
hesabu na tukaamua tuweke kiwango hicho kwa ajili ya wakazi hao,” alisema.
Alisema
katika mikoa mikoa mingine gharama za kuunganisha umeme ni sh. 177,000/- lakini
kwa mikoa ya Lindi na Mtwara gharama hizo zilishushwa na kufikia sh.99,000/-.
“Lakini sasa hawa wenzetu tumewapa upendeleo zaidi na tumewapunguzia gharama
hizo hadi sh. 27,000/-,” alisema huku akishangiliwa.
hayahaya watanzania habari ndiyo hiyo
ReplyDelete