![]() |
| Waziri mkuu wa tanzania.MH: mizengo pinda |
“Katika
hili tulizidiwa ujanja na watu wengine kwa kuwa walikuwa wakiwaambia wananchi
kwamba gesi itatolewa Mtwara na kupelekwa Dar es Salaam.
“Tena
wakasema ikishafikishwa Dar es Salaam ambako vitajengwa vinu na gesi nyingine
itapelekwa Bagamoyo kwao Rais Jakaya Kikwete.
“Huo
ulikuwa ni upotoshaji mkubwa tena mkubwa kweli lakini sisi tulilichukulia juu
juu, hatukutazama kwa undani kulieleza hilo na wajanja wakalipata na
kulipotosha hilo,” alisema Pinda.
Alisema
gesi itazalishwa Mtwara ingawa vinu vitajengwa Dar es Salaam kwa ajili ya
kuisambaza gesi hiyo kwa watumiaji wengine.
“Wakati
nazungumza na watu wa Mtwara mwaka jana, walinieleza mambo mengi sana juu ya
hiyo gesi na mwishowe nikawauliza hivi kwanini hamtaki gesi itoke Mtwara.
“Nikawauliza,
hivi ikija meli hapa Mtwara ikapaki pale bandarini na kupakia gesi na kuipeleka
Uarabuni mtakataa, wakasema hatuna shida, nikawauliza tena je, meli hiyo hiyo
ikipakia gesi na kuipeleka Dar es Salaam, mna tatizo, wakasema hatuna tatizo.
“Sasa
nikawauliza tatizo lenu ni nini, wakasema ni hilo bomba lenu hilo mnalojenga.
Mimi nikawaambia gesi itazalishwa hapa Mtwara, tena katika Kijiji cha Madimba
na itakayopelekwa Dar es Salaam haitazidi asilimia 10.
“Nikawambia
gesi ikianza kuzalishwa mtanufaika kwa kuwa hata viwanda vitakuwapo kikiwamo
cha Dangote kitakachozalisha saruji pale Kijiji cha Msijute,” alisema Pinda.
Kuhusu
hasara iliyopatikana baada ya wananchi kufanya vurugu na kuharibu mali, alisema
bado inafanyiwa kazi na itakapokamilika italetwa mkoani Mtwara.
“Baada
ya vurugu zile, Serikali ilifanya tathimini ya matukio na ikiwezekana kabla ya
mwisho wa mwaka wa fedha huu itakuwa imekamilika na tutaangalia la kufanya
ingawa nataka niwahakikishie kwamba jambo hili tunalifanyia kazi na
litakapokamilika tutalirudisha kwenu,” alisema Pinda.
Aliwashukuru
viongozi wa Mkoa wa Mtwara kwa kutochukua uamuzi wa kulipa kisasi wakati wa
vurugu hizo kwa kuwa kama wangeamua kufanya hivyo hali ingekuwa mbaya zaidi.
Awali,
Mkuu wa Wilaya ya Masasi, Farida Mgomi, alisema vurugu hizo zilizotokea Januari
26, 2013 zilisababisha hasara ya Sh bil 3.4.
SOURCE:Mtanzania
SOURCE:Mtanzania

No comments:
Post a Comment