SERIKALI ya wilaya ya Igunga mkoa wa Tabora imefanikiwa kuhamasisha jumla ya vitongoji 624 kujiunga na mfuko wa afya ya jamii (CHF). Mkuu wa wilaya ya Igunga Elibarik Kingu alisema hayo katika kikao cha wadau wa mfuko wa afya ya jamii tiba kwa kadi (TIKA) kilichofanyika mkoani Tabora. Alisema licha ya kuvifikia vitongoji hivyo pia wamepania kufikisha idadi ya wanachama wanaopata huduma ya mfuko huo 20,000 ifikapo mwaka 2014. Kingu aliongeza kuwa kufikia malengo bado kunahitaji watendaji waadilifu na kwamba Igunga imefanikiwa kwenye huduma za afya hasa kutokana na kuwepo watendaji wanaojituma na waadilifu. “Watendaji sisi tunapaswa kubadilika…..tatizo tumekuwa tukikiongea sana,siasa na kufanya kazi kwa mazoea tukubali kubadilika.”aliongeza. Alisema ifikie mahali sasa viongozi wa chi yetu tuwe wa mfano na kuongoza wananchi wetu. Aidha aliwataka viongozi wa Tabora manispaa kuacha tabia ya kukomoana na badala yake wanapaswa kumtumia mkurugenzi wa sasa Alfred Luanda ili mji wa Tabora ufanikiwe. Kwa upande wake mkurugenzi wa manispaa Tabora Alfred Luanda ambaye mfuko wa Taifa wa bima ya Ayfa ulikuwa ukizindua na kupitisha sheria ya huduma ya tiba kwa kadi TIKA katika manispaa Tabora,alisema amefarijika sana huduma hiyo kuanzishwa. Luanda alisema ili kufanikiwa ameomba watendaji kuacha tabia ya kufanya kazi kwa kukomoana,majungu na fitna. Alisema kazi waliyopewa ni ya wananchi hivyo kuwepo visasi,majungu na kukatishana tamaa hakutaisadia manispaa Tabora. Alitaka watendaji kuchukua hatua za kiutendaji na siyo kufanya kazi kwa faida ya kiongozi fulani kwani ni hatari.
EBENEZA MARCH 9 2014
SWACO
royal
tt
NIMO
mvuto
Sunday, January 19, 2014
IGUNGA YAHAMASISHA VITONGOJI 624 KUJIUNGA CHF.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment